HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2022

SOS Childen's Village yapongezwa kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa mtoto

 

NA MWANDISHI WETU

 

AFISA Maendeleo ya Jamii kutoka Jiji la Dar es Salaam Daudi Mpoli ameishukuru SOS Childen's Village kutokana na kuisaidia serikali katika mapambano ya kuondoa ukatili dhidi ya mtoto.

Mpoli amebainisha kuwa SOS Childrens Village imefanya kazi kubwa katika ngazi mbalimbali za  Wizara,Mkoa,Wilaya na Kata na kuwataka wale wote wanaoweshwa kuendeleza miradi hiyo ili iwe endelevu.

Mpoli ametoa kauli  hiyo leo Chanika jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa vikundi vya huduma ndogo za kifedha zaidi ya 30 vinavyo jishughulisha na masuala ya kupinga ukatili kwa mtoto.

 

Vikundi hivyo ambavyo vipo chini ya Mradi wa Kuimarisha Familia na Ustawi wa Mtoto kutoka SOS Childrens Village unahusisha  Kata za Chanika na Zingiziwa zilizopo Jiji la Dar es Salaam ambapo pia vimefanikiwa  kuunda Umoja wa Usimamizi wa Mfuko wa Mtoto (UWAMTO)

 

Akizungumza na viongozi wa vikundi hivyo,Mpoli amefafanuwa kuwa  SOS Childrens Village ipo siku itaondoka lakini jamii itaendelea kuwepo hivyo ni lazima kuwa na mifumo endelevu ya miradi na kazi zinazotolewa na SOS Childrens Village.

“Nawapongeza sana juu ya kufanikiwa kuanzisha mfuko huu wa watoto katika Kata za Zingiziwa na Chanika lakini lazima mfanye kazi kisasa kwa kushirikiana na serikali kwani watu wanaopata mahitaji kutokana  taasisi mbalimbali wapo wengi lakini Balozi na Afisa Maendeleo wa Kata wanajua taasisi na idadi ya watoto wanaosaidiwa katika eneo husika.

“Sisi kama serikali mikopo ipo katika vikundi kama hivi ili kutunisha mfuko huo kwani kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kuweka mfumo bora kwa vikundi kupata mikopo  bila mlolongo”amesema Mpoli

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Development Concern linalofanyakazi kwa kushirikiana na SOS Childrens Villages (DECO) Robert Nyampiga amesema wamekutana na vikundi hivyo ili kutoa mwongozo  na kutatua changamoto zinazohusina na uendeshaji wa mfumo huo wa UWAMTO.

Amesema SOS Childrens Village ni mwezeshaji na mlezi wa vikundi  32 na wao kama DECO ni wawezeshaji  ambapo vikundi hivyo licha ya kuwezeshwa kufanya masuala ya ujasiriamali ili kujiongezea kipato lakini pia kuendelea na shughuli za kupinga ukatili dhidi ya mtoto.

Nyampiga amebainisha kuwa mradi huo ulianza baada ya SOS Childrens Village kuona ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto hivyo kuamua kuuanzisha ambapo  umesaidia kupunguza vitendo hivyo kwa asilimia 80 katika Kata hizo.

 

Naye Mwenyekiti wa UWAMTO Shirazi Sinde  amesema changamoto waliyonayo kwa sasa ni uendelewa mdogo kwa wananchi juu ya UWAMTO kwa kuwa wao kama jamii wamekuwa wakisaidia watoto pindi wanapofanyiwa ukatili.

 

Mwakilishi wa Kikundi cha Tuwezeshane Maonesho Rashidi amesema SOS Childrens Village wamefanya kazi kubwa ikiwemo kuchimba visima,kujenga madarasa na kusaidia watoto hasa katika kuibua ukatili dhidi ya watoto.

“Serikali inahuruma lakini tungeomba SOS Childrens Village wasimamie wenyewe ikiwemo kusimama mahakamani kutoa ushahidi maana kazi waliyoifanya imesaidia sana kupungua kwa vitendo vya ukatili kwa watoto katika eneo hili tofauti na ziku za nyuma”amesema Maonesho

 

No comments:

Post a Comment

Pages