HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 04, 2022

TTCL yapongezwa maonesho ya Nane Nane jijini Dodoma

 
Na Mwandishi Wetu.


WATANZANIA wametakiwa  kuzingatia  maadili ili kuweza kujenga watu wenye  uzalendo na nchi ikiwamo katika kulinda, kutunza rasilimali za Taifa ikiwemo miundo mbinu ya mawasiliano ambayo ndiyo kiungo muhimu katika nyanja ya usalama.


Rai hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Ofisa Mkufunzi Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Faustine Malecha alipotembelea Banda la  Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya Wakulima  nanenane.

Maonyesho ya nanenane yanaendelea katika viunga vya Nzuguni, jijini  Dodoma.
 
Malecha aliyekuwa ameambata na Wanafuzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosoma Falsafa na Maadili walioko katika mafunzo ya vitendo ofisi ya Takukuru  Dodoma, ameipongeza TTCL kwa hatua kubwa iliyofikia katika kuhakikisha linarejea na kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi wake.


"Mtazamo niliokuwa nao kuhusu TTCL na baada ya kufika bandani hapa,  maofisa niliowakuta waliotumia utaalam wao kuelezea shughuli kubwa zinazofanywa na shirika hilo, nimebaini kuwa maendeleo makubwa yameongezeka ikilinganishwa na lilivyokuwa hapo awali". Alisema Malecha.

No comments:

Post a Comment

Pages