Mchezaji wa Pooltable, Abdul Faraji kutoka timu ya Fuoni Zanzibar akicheza dhidi ya mpinzani wake Mohamed Idd wa timu ya Y2K(hayupo pichani) wakati wa fainali za Mkoa wa kimichezo wa Ilala wa kufuzu kucheza fainali za Kitaifa zililizomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Nderingo Tabata jijini Dar es Salaam.Timu ya Y2K ilishinda 13 – 12 na hivyo kuwaa Ubingwa wa Ilala pamoja na kufuzu kushiriki mashindano ya Kitaifa ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika Agosti 20 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa wa ndani.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya mchezo wa Pooltable ya Y2K yenye Makazi yake Buguruni Ilala jijini Dar es Salaam imeibuka Bingwa katika mashindano ya Pool ya Mkoa wa Kimichezo wa Ilala kwa kufunga timu ya Fuoni kutoka Zanzibar 13 – 12 na hivyo kufuzu kuiwakilisha Ilala kwaenye fainali za mashindano ya Pool ya Nane nane yajulikanayo kama “88” Pool Competitions 2022 yanayotarajiwa kufanyika Agosti 20 mwaka huu katika Uwanja wa ndani wa Taifa.
Timu ya Fuoni pamoja nna kufungwa ilikamata nafasi ya pili hivyo nayo ifuzu kupata nafasi ya kushiriki fainali za Kitaifa hapo Taifa.
Timu ambazo zilishiriki lakini hazikufuzu ni ni Mashujaa yenye makazi yake Vingunguti na Never Give Up yenye makazi yake Ubungo Exterbal.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Wanaume, Salim Yusuf kutoka timu ya Fuoni Zanzibar alitwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa kumfunga Abdul Faraji 9 – 3 na hivyo kufuzu kushiriki fainali za Nane nane 2022.
Washindi wengine wa upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) waliofuzu kushiriki fainali za Nane nane 2022 ni Abdul Faraji aliyekamata nafasi ya pili , Mohamed Idd aliyekamata nafasi ya tatu, na Rashid Yahaya aliyekamata nafasi ya nne pamoja na wachezaji wane ambao walifanikiwa kuingia robo fainali ambao ni, Hussein Amir, Geofrey Muyaga, Isaya Paulo na Ramadhani Killer.
Upande wa Mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Cecilia Kileo alichukua Ubingwa huo kwa kumfunga Judith Machafuko 5 - 0 na hivyo kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za Nane nane 2022.
Judith Machafuko kwa kuchukua nafasi ya pili lakini pia nae alifuzu kushiliki kucheza mashindano ya Nane nane 2022 kwani nafasi zilizokuwa zinahitajika kwa Wanawake ni Mbili tu.
Akizungumya Mratibu wa Mashindano ya Nane nane “88” Pool Competitions 2022, Michael Machela alisema, Fainali za Mashindano ya Nane nane 2022 zitafanyika Agosti 20,2022 katika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kukamilisha mzunguko wa Mashindano ya hatua ya Miko.
No comments:
Post a Comment