HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2022

ZECO - Wafanyakazi kufukuzwa

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Joseph Kilangi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).


 Na Salma Lusangi

 

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) watafukuzwa kazi endapo uchuguzi unaoendelea ukibaini wameshiriki katika kuwaunganishia umeme watu waliyokamatwa kwa kosa la kujiunganishia umeme kinyume na sheria huko eneo la Chukwani Zanzibar.

 

Kauli hiyo imeitowa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Joseph Kilangi wakati akizungumza na watendaji wa ZECO katika ofisi ya shirika hilo jana, alisema mwananchi wa kawaida aliyekuwa hajasoma fani ya umeme hawezi kuchezea umeme lazima alishirikiana na mtaalamu wa umeme kutoka ZECO au nje ya ZECO hivyo ripoti ya uchunguzi ikionesha mtendaji wa Shirika la hilo amehusika atamfukuza kazi.

 

“Mimi ninavyofahamu nguzo ya umeme haikai ndani ya fensi, kuna mtu hapo amecheza aidha kuungana na mfanyakazi wa ZECO na mfanyakazi yeyote aliyeshiriki kuungana na kishoka hatakuwa salama nitamchomoa! Sasa ni vizuri ajitokeze mwenyewe tujuane nani aliyesababisha hayo. Kaduara operasheni imewakamata watu wawili wanatumia umeme kwa kujiungi wenyewe kutoka kwenye nguzo” alisema Kilangi.

 

Katibu Mkuu huyo aliwataka Mwasheria wa Shirika hilo kufikisha kesi ya watu  waliyokamatwa kwa kosa kujiunganishia umeme kinyume na sheria mahakamani pamoja na kuifuatilia kwa kina kwasababu ni kosa la kuhujumu uchumi.

 

Aidha aliwataka watendaji wa Shirika hilo kuongeza kazi ya utendaji katika kuwahudumiwa wananchi ikiwemo kuwaungia umeme kwa haraka wakati mtu ameshalipa malipo yanayotakiwa asihangaishwe na kupewa siku kadhaa za kusubiri huduma ya umeme.

 

Pia alisema wahudumu wanaotoa umeme katika vituo mbali mbali vya Unguja na Pemba wapangwe vizuri katika vituo hivyo vya umeme. Kila dirisha litowe huduma kwa wateja na sio litumike dirisha moja huku mhudumu mwengine akikaa kwenye mkeka kwa kisingizio cha kukosekana kwa mtandao (Internet).

 

Mwisho aliwaomba watendaji hao kuendeleza mashirikiano ndio yatakayoleta maendeleo kwa Shirika hilo katika kuwafikishia wananchi umeme mjini na vijini ndio lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

 

Nao wafanyazi wamemuomba Katibu Mkuu huyo kuwahimiza watendaji Wizara ya Fedha kuhusu ununuzi wa magari kwani wameshafanya taratibu zote zilizohitajika. Pia wameomba Shirika kuongeza rasilimali watu ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

 

Watu wanaotuhumiwa kuiba umeme eneo la Chukwani Zanzibar walikamatawa kupitia zoezi maalumu lilopewa jina la Kaduara operasheni) lilofanyika siku ya Agosti 3, 2022. Watu hao walichukuliwa na jeshi la Polisi Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

Pages