HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2022

AYE kupeleka Vijana nane kucheza soka Uturuki, Georgia na Azberjan

 



Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Kampuni ya Arts Youths Empowerment (AYE) kupitia Programu ya AYE Ibua Viapji 2022 inatarajia kupeleka vijana nane kwenda kucheza soka katika nchi za Georgia, Ututruki na Azberjan.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mipango na Utawala wa AYE, Lairumbe Laizer amesema mwaka 2018 walianzia ngazi za chini kutafuta vipaji vya soka vya vijana na baadae walifikria kupanda ngazi za juu kwa kutafuta wadau ili kutengeneza hatma ya soka la nchi.

" Lengo la programu hii ni kuhamasisha, kuibua na kuendeleza vipaji, kuinua uchumi wa mtu binafsi na kuitambulisha nchi wazazi wahamasisheni watoto kwenye viapji vyao watimize ndoto zao, amesema Laizer.

Amebainisha kuwa vijana nane kwa mpigo wanaenda katika nchi hizo kuongezewa ujuzi na kwamba progarmu ya mchujo wa kupata vijana wengine itafanyika Juni 25 mwaka huu katika Viwanja vya Magereza Ukonga.

Kwa upande wake Kocha, Hadji Shaban amesema vijana waliochaguliwa wanatarajia kuanza safari kuanzia Mei 3 hadi 13 kuelekea katika nchi hizo huku akilishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini( TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kutoa ushirikiano uliosaidia kuwapata vijana.

Nae, Skauti wa AYE, Firat Totik amesema walifanya skauti ya kutafuta vijana hao Zanzibar na Tanzania Bara na kwamba kati yao wapo wanaokwenda Uturuki, Georgia na Azberjan kwenye timu za ligi kuu.

Miongoni mwa vijana waliopata nafasi hiyo, Ramadhan amesema amefurahi kupata usaili AYE na anaamini atatimiza ndoto za kuwa mchezaji bora na kulisaidia taifa kupata wachezaji wa nje wenye uzoefu.

Mzazi Issa Juma ameishukuru AYE na kuamini mtoto wake ataitendea haki nafasi aliyoipata na kuiomba iendele na mpango wa kuhakikisha wanasaka vipaji

No comments:

Post a Comment

Pages