HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2022

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAKUTANA NA UONGOZI WA WAKALA WA KUUZA VIFAA VYA ZIMAMOTO


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga, akimsikiliza Mwenyekiti wa TAFEDA Bwa. Hamisi Balowa (mwenye suti Nyeusi) wakati akiwasilisha taarifa na changamoto zinazokikabili chama hicho, mapema leo tarehe 2 Septemba, 2022 walipokuwa kwenye kikao Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia kwake ni Kamishna wa Utawala na Fedha Mbaraka Semwanza”ndc” na Kushoto wake ni Kamishna wa usalama kwa Umma Jesuald Ikoko.

 

Mapema leo Septemba 02, 2022, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekutana na Uongozi wa wauzaji na wasambazaji wa Vifaa vya kuzimia moto “Fire Dealer” kupitia chama chao cha TAFEDA na kujadili mambo mbalimbali kuhusu Moto na Maokozi zikiwemo changamoto zinazo wakabili katika utendaji wao.

 

Akiwasilisha changamoto hizo kwa kamishna Jenerali, Mwenyekiti wa TAFEDA Hamisi Balowa amesema wanakabiliwa na ukosefu wa Wataalamu wenye ujuzi wa elimu ya sayansi ya Moto na Maokozi kwa sababu gharama za kulipia masomo hayo yanayotolewa na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji ziko juu sana.

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, amewahakikishia Viongozi hao kuzifanyia kazi changamoto hizo kama ambavyo serikali imefanikiwa kuwashushia Tozo ya uwakala wa uuzaji na usambazaji wa vifaa vya kuzimia moto.


 “Ninyi ni sehemu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu kazi mnazozifanya mnasaidia kuimarisha Usalama wa Watu na Mali zao pamoja na Kuokoa Maisha”. Alisema CGF Masunga.

 

 Aidha Kamishna Jenerali Masunga, amewahaidi kuzitatua changamoto zao na kuwataka wajitangaze kwani jamii haijui uwepo wao pamoja na huduma wanazozitoa, kwani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji halijihusishi na uuzaji na usambazaji wa bidhaa hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages