NA MWANDISHI WETU
BIMA ni njia ya ulinzi wa kiuchumi dhidi ya hasara ya kifedha au
hata dhidi ya kifo ambayo watu au kampuni wanafuata kwa kulipa kiasi
fulani kwa shirika la bima kwa mkataba maalum. Kuna aina mbalimbali za bima
kuna bima ya afya, bima ya nyumba, bima ya vyombo vya moto, bima ya maisha na
bima ya ulemavu.
Bima ya afya
Bima ya afya humsaidia mwanachama aliekata bima hiyo kupata matibabu na dawa
endapo atapata matatizo ya kiafya ama maradhi mbali mbali.
Bima ya nyumba
Bima ya nyumba humsaidia mkata bima endapo atapata matatizo ya huaribifu wa
nyumba yake kama moto na athari zingine, basi shirika hilo la bima litamlipa
ama kufidia hasara iliotokea na kama huaribifu ni mkubwa zaidi na kufanya
nyumba hiyo kuteketea kabisa basi shirika hilo la bima litampatia nyumba
nyingine.
Bima ya vyombo vya moto
Bima hii humsaidia mkata bima ama mwanachama kulipwa fidia endapo chombo chake
kitapata matatizo ama huaribifu na aina ya vyombo hivyo vya moto ni magari,
bajaji na piki piki. Endapo gari yako itapata huaribifu mkubwa sana na
kushindwa kutengenezwa basi utalipwa pesa yenye thamani ya gari yako.
Bima ya maisha
Bima ya maisha ni aina ya bima ambayo huhusika zaidi na kuwalipa watu walio
orodheshwa na mtu aliekata bima kama wanufaika pindi anapoaga dunia ama
kufariki.
Bima ya ajali
Bima ya ajali humsaidia mwanachama kulipwa fidia endapo atapata matatizo yalio
sababishwa na ajali mfano ulemavu wa kudumu na matatizo mengine.
Nini maana ya uwekezaji?
Uwekezaji ni nyongeza ya mali inayoingiza mapato. Mali hizi ni zile ambazo zina
wigo wa kuthaminiwa zaidi, thamani yao huongezeka kwa muda na kuwa chanzo cha
mapato kwa mwekezaji. Ama kwa lugha nyepesi uwekezaji ni namna ya kufanya fedha
zako ziweze kuzaa fedha zingine.
Ili uweze kuwekeza una hitaji kuwa na chanzo cha mapato kama biashara ama
ajira hata kama ni kidogo, fedha ama pesa unayoipata kwenye chanzo hicho
basi unatenga kiasi kidogo na kuwekeza ama una weka akiba kidogo kidogo na
badae ikifika kiwango fulani unawekeza.
Je! Vipi endapo utapata mfumo ambao utakupa nafasi ya kupata bima na
uwekezaji kwa pamoja? basi UTT AMIS kupitia mfuko wake wa wekeza maisha ni jibu
la swali hili.
UTT AMIS ni taasisi ya serikali inayofanya uwekezaji wa pamoja ilio chini ya
wizara ya fedha na mipango. UTT AMIS ilianzishwa mwaka 2005 na imefanya na
inaendelea kufanya kazi nzuri ya uwekezaji wa pamoja hadi sasa, na kwa kipindi
chote icho kuanzia 2005 hadi sasa 2022 iliunda ama kuanzisha mifuko mbali mbali
ya uwekezaji wa pamoja, moja ya mifuko hiyo ni wekeza maisha.
Uwekezaji wa pamoja ni nini?
Uwekezaji wa pamoja ni mfumo unao lenga kukuza mitaji ya wawekezaji na kutoa
nafasi kwa mtu ama watu wenye nia ya kuwekeza hata kama wana kiwango kidogo cha
pesa.
Mfuko wa wekeza maisha ulianzishwa mwaka 2008 kwa lengo la kukuza mitaji ya
watanzania pamoja na kutoa bima.
Mfuko huu tangu umeanzishwa umekua mara saba
hii inamaanisha aliweka elfu kumi sasa ana elfu sabini, alieweka laki moja sasa
ana laki saba, alieweka milioni moja sasa ana milioni saba, alieweka milioni
mia sasa ana milioni mia saba nk. Mpaka sasa mfuko una thamani ya bilioni 5 za
kitanzania. Mfuko wa wekeza maisha umetoa nafasi ya uwekezaji kwa Watanzania
wenye umri wa miaka 18 hadi 55.
Mwekezaji anafaidikaje na mfuko wa wekeza maisha?
Ukiwekeza kwenye mfuko huu utapata faida ya kuongezeka kwa mtaji wako
nikimaanisha pesa unayoiweka ama kuwekeza kwenye mfuko huu inaongezeka taratibu
taratibu na kwa muda mrefu hutengeneza faida nzuri, na pia utapata bima.
Kuna bima za aina mbili kuna bima ya maisha pamoja na bima ya ajali ambayo
itakusababishia matatizo kama ulemavu wa kudumu.
Mfuko huu una kiwango cha chini cha uwekezaji pamoja na ukomo wa faida za bima,
kiwango cha chini cha uwekezaji ni shilingi milioni moja kwa kipindi chote cha
uwekezaji, na unampa mwekezaji nafasi ya kuchagua mpango wa kuiweka pesa hiyo
kidogo kidogo au kuiweka kwa mkupuo. Ukomo wa faida za bima kwenye mfuko huu ni
shilingi milioni 25 kwa kipindi chote cha uwekezaji hii inamaanisha hautolipwa
zaidi ya milioni 25 kama utapata matatizo.
Akipata ulemevu wa kudumu (kupoteza uwezo wakuona macho yote mawili, kupoteza
mikono ama miguu yote miwili, kupoteza uwezo wa kusikia masikio yote mawili.)
atalipwa fidia ya asilimia 100.
Mwekezaji akifariki mrithi wake au warithi wake aliowaorodhesha Bima itamlipa
mwekezaji kuanzia asilimia 5 hadi 100 ya milioni 25 kulingana na tatizo husika.
watalipwa pesa yote aliochangia na faida zilizo zalishwa na kama mwekezaji
alifariki kabla ajamaliza uwekezaji wake ama kiwango alichosema atawekeza kwa
kipindi chote cha uwekezaji basi kile kiwango ambacho hakufanikiwa kukimaliza
ama kuwekeza mrithi au warithi wake watapewa, kwasababu taasisi ya UTT AMIS
inaamini kua mwekezaji kama angepata nafasi yakuwekeza angeweza kumaliza
kiwango chake cha uwekezaji kwa muda wote huo.
Mfuko huu pia una gharama za mazishi ambazo ni 500,000 na pesa hii atapata
mrithi ama warithi wa mwekezaji pale anapowasilisha kibali cha mazishi kwenye
ofisi za UTT AMIS, na pesa hiyo italipwa kwa mrithi ama warithi walio
orodheshwa na mwekezaji.
Pesa zitakazokua zinatoka kulipa fidia ya tatizo lililotokea ni pesa za bima na
sio pesa za mwekezaji alizowekeza kwenye mfuko, asilimia 99 ya pesa ya mteja
itawekezwa na asilimia 1 tu ndo itaenda kulipa gharama za bima.
Mfuko huu unamuda wa kuwekeza ama uwekezaji. Mwekezaji akiwekeza kwenye huu
mfuko itambidi akae kwenye huu mfuko kwa kipindi cha miaka kumi.
Unaweza kuona miaka kumi ni mingi ila kwa mtu mwenye malengo ya muda mrefu na
mwenye nia ya uwekezaji basi kwake hatoona kama ni miaka mingi bali ataona
fursa ya kupata nafasi ya kuwekeza kwa muda mrefu na kutengeneza faida nzuri
zaidi.
Mwekezaji akimaliza kipindi chake chote cha uwekezaji atapata mkono wa pongezi
kutoka UTT AMIS wa asilimia 5 na asilimia 7, mwekezaji atapata asilimia 5
endapo alikua anawekeza kidogo kidogo kufikia kiwango chake alichosema na
mwekezaji atapata asilimia 7 kama aliweka pesa hiyo kwa mkupuo ama kuweka kiasi
chote cha pesa kwa pamoja.
Naomba nikueleweshe vizuri asilimia tano na saba sio ya pesa uliowekeza tu kwa
miaka kumi bali ni pesa yako uliowekeza na faida zilizotengenezwa kwa miaka
yote kumi. Tunajumlisha pamoja na kupata kiwango kamili cha pesa zako kwa muda
wote wa uwekezaji alafu tunakupa asilia tano au saba tena kama mkono wa pongezi
kwa kutimiza malengo yako uliojiwekea miaka kumi nyuma.
No comments:
Post a Comment