Makamu Mwenyekiti wa CCM)Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wanachama wa CCM katika mkutano wa ndani akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Na Mwandishi Wetu, Geita
MAKAMU Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu amewashauri
wabunge na madiwani wa Chama hicho kuwa wakali katika kuisimamia
Serikali ili itekeleze ahadi za miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Kinana
alitoa kauli hiyo jana mbele ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
aliokuwa anazungumza nao kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika
Ofisi ya Chama hicho.
Alikuwa akielezea kwa kina namna ambavyo
kuna baadhi ya miradi ikiwemo ya maendeleo ambayo inatengewa fedha
lakini fedha hizo zinaelekezwa sehemu nyingine.
“Mimi ni mmoja wa
watu ambaye ninapenda Wabunge wawe wakali kidogo kuhusu mambo ya
Serikali, sio wakali kwa maana ya kuisakama Serikali lakini wawe wakali
kwa kuiwajibisha serikali.
“Unajua hiki Chama ndicho
kinachokwenda kwenye Uchaguzi , hiki Chama ndicho kinachoomba kura, hiki
Chama ndicho kitakachopewa viongozi au kitakachonyimwa sio
Serikali.Wale watendaji na watumishi wa Serikali wao wapo tu, wewe
ukiwepo wao wapo, ukiondoka wao wapo,”alisema Kinana.
Aliongeza
kuwa iwapo mambo hatakwenda watakaodhibiwa ni Chama Cha Mapinduzi ,
hivyo amewasihi lazima wana CCM wakiwemo madiwani na wabunge kuwa
wakali.“Ndugu zangu nataka niwasihi sana lazima tuwe wakali na mambo ya
wananchi, mambo yetu binafsi hatutakuwa wakali lakini mambo ya wananchi
lazima tuwe wakali.”
Amefafanua hivyo katika kusimamia masuala
yanayohusu maendeleo ya wananchi mbali ya kuwa wakali ni wajibu wa kila
mmoja kwenye nafasi yake akatimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na
kumsaidia Rais katika kufanikisha malengo yake ya kuwatumikia wananchi
na kuwaletea maendeleo.
“Rais anajitahidi sana lakini Rais hayuko
peke yake, Rais nchi hii si mali yake na katika uongozi lazima atumie
taasisi, atumie taratibu, kanuni, sheria pamoja na sera na sisi wote
tumsaidie Rais ili aweze kufanikiwa. Mmesema hapa(Geita)Rais ametoa
fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo.
“Ametoa hiki, amesaidia
kile lakini peke yake hawezi lazima Bunge, Kamati za Bunge, halmashauri,
wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri wasaidie na kila mmoja wetu
asaidie upande wake.Hivyo tunaowajibu mkubwa sana,”alisisitiza Kinana.
Alifafanua
kuwa CCM ndio inayopita na kuahidi wananchi kupitia Ilani kuhusu
yatakayofanyika hivyo ahadi zinaposhindwa kutekelezwa wakati fedha
zimetengwa wapinzani wanapita na kueleza CCM ahadi zao ni hewa.
“Kwa
hiyo hapa Geita kwenye hili la ombi la kutengenezewa barabara
nimejifunza na katika ziara zangu mikoa niliyokwenda nimekutana na hii
la miradi kusua sua kwasababu ya fedha zinatengwa halafu
hzipo,”aliongeza Kinana.
Akieleza zaidi kwenye hilo alisema
atakwenda kukaa na Waziri wa Ujenzi ili amuulize swali kwamba ameona
barabara fedha zinatolewa halafu baadae wanasema hazipo.
“Nilikuwa
huko Rukqwa, Katavi na sasa hapa nyie (Geita) habari ndio hiyo hiyo,
hata kama huna uwezo wa kutoa fedha zote basi toa kiasi fulani halafu
tujue kwamba umeshindwa lakini uwaambie fedha hizi ilikuwa tutoe lakini
zimekwenda mahala kwingine, hilo sio jambo jema sana.
“Na mengine
ni kuzungumza na Mawaziri kama tunatoa fedha za barabara na tuangalie
na mikoa ambayo haina barabara nyingi za lami, wale ambao barabara zao
nyingi ni za lami basi kidogo wacheleweshwe na wale ambao hawana
barabara za lami nyingi fedha ziende maeneo hayo.Sio maneno mazuri ya
kusema lakini ni maneno ya ukweli,”alisema Kinana.
Alifafanua
kuna mikoa ukienda barabara za lami ziko kila mahali lakini ukienda
mikoa mingine unakuta hakuna barabara nyingi za lami lakini wakati wa
kupanga bajeti za barabara za lami na kule kwenye barabara za lami.
KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI GEITA
Katika
hatua nyingine Kinana alizungumzia migogoro ya ardhi mikoani Geita
baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Mkoa ambayo imeteja eneo hilo kuwa
na changamoto ya migogoro na kuomba Chama hicho kusaidia kumaliza
migogoro hiyo.
“Mkuu wa Mkoa wa Geita jana na leo tumezungumza ,
nadhani hili jambo ni muhimu sana na lazima ifike mahali liishe, nchi
hii ina migogoro mingi sana ya ardhi, kila mahali ardhi ardhi.Juzi
nilikuwa Kigoma tulifanya mkutano kuanzia saa tisa mpaka saa 2:30 usiku
na wana CCM.
“Nusu ya muda tumezungumzia ardhi na mgomvi mkubwa
ni ardhi , ardhi, ardhi, sasa lazima tufike mahali tupate ufumbuzi, hapa
kwenu(Geita) mna matatizo na misitu, mgororo kati ya wananchi na misitu
, mgororo kati ya wananchi na hifadhi.Mgogoro huu sio wa leo.
“Mimi
nikiwa Katibu Mkuu wa CCM na nilipita kote huko nimeiukuta .Rais amekua
ameunda timu na imekuja hapa , mkuu wa Mkoa ameniambia imefanya kazi
nzuri lakini kuna sehemu wameacha.Nitaandika kwenye taarifa zetu na
kupeleka kwa Rais.
“Kuna wale watu uliowatuma kule
hawajafika kila mahali halafu mtu anaulizwa mbona hamjafika kila mahali
anajibu kumbe nimesahau.Sasa unasahau vipi wakati umetumwa na Mkuu wa
nchi.Kwa hiyo lazima tutafute namna ya kupata ufumbuzi wa
kutatua,”alisema.
Kinana alisema katika kushughulikia migogoro ya ardhi ni lazima wazungumze na Kamati za Ardhi ya Bunge ili isaidie.
MIKOA YENYE UKAME NA UPANDAJI MITI
ndugu
mkuu wa mkoa nataka niombe hii mikoa ambayo inaukame ukame kidogo
kwanini msitengeneze mkakati wa pamoja sijui kama mnao, mpande miti,
unajua hii nchi ina bahati kubwa sana ya kuwa na kiongozi mmoja
aliyekuwa mzuri sana .
Na kila jambo alikuwa vizuri,
anaitwa Mwaliju Julius Nyerere kuna mradi hapa wengi wenu hamuujui
kwasababu ya umri wenu ni mdogo, kuna ulikuwa unaitwa HASH ni mradi wa
kupanda miti kwenye mikoa ya mwanza, Shinyangi na wakati huu Geita
,Simiyu kwasababu ya ukame , na fedha zikatafutwa nje na mwalimu nyerere
alikuwa na kauli mbiu panda mti, kata mti .
Kwa hiyo
mnatakiwa kupanda miti kama vichaa lakini ili mpande miti lazima muwe na
mikakati, muwe na vitalu vya miti , lazima muwagawie wananchi wenu miti
waweze kupanda sasa mimi ningeomba hii mikoa yenye ukame kuwe na
mkakati wa pamoja mpange ma rc, mwite waziri wa misitu sijui kama waziri
wa misitu anapanda miti au kazi yake ni kupambana na wananchi kwenye
misitu, kazi ya waziri wa misitu namba iwe kupanda miti mwalimu
alianzisha ule mradi na mwenyewe akawa mstari wa mbele.
No comments:
Post a Comment