Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Richard Kayombo.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/23
imepanga kukusanya Sh Trillioni 23.65 ambayo ni sehemu ya bajeti ya
Serikali ya Sh Trilioni 41.48 huku ikibainisha kufanikiwa kukusanya Sh
Trillioni 22.99 mwaka wa fedha 2020/21.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Richard Kayombo wa
mamlaka hiyo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam
kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2022/23.
Amesema
kuwa katika kuhakikisha wanafikia malengo ya makusanyo waliyojiwekea
katika mwaka fedha hu tayari wameshaanza kwa kasi ya kuelimisha
watumishi na wafanyabiashara wote juu ya mabadiliko ya sheria mbalimbali
za kodi, tozo na ada zinazosimamiwa na TRA pamoja na taratibu za
ukusanyaji na usimamiaji mapato ya Serikali.
"
Lengo ni kuhakikisha kuwa sote watumishi na walipakodi tunakuwa na
uelewa mmoja ili kurahisisha ukusanyaji na ulipaji kodi kwa hiari wakati
wote, marekebisho ya sheria za kodi yamelenga kusaidia kuongeza kasi ya
kufufua uchumi na kuimarisha sekta za uzalishaji kwa ajili ya
kuboresha maisha," amsema Kayombo.
Amebainisha
kuwa wamejipanga kimkakati kufanikisha lengo la makusanyo waliopangiwa
kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuongeza usiamamizi wa utoaji
risiti kwa njia ya Mashine za Kielektroniki pamoja na kuziba mianya
undanganyifu.
Amesisitiza kuwa TRA inaimarisha
mifumo iliyopo pamoja na kuzindua mifumo mipya ya kukusanya kodi
mbalimbali ili kuongeza ufanisi, urahisi wa ulipaji kodi na ukusanyaji
pamoja an kuokoa muda wa gharama kwa mlipakodi na mamlaka hiyo.
Ameongeza
kuwa wamejipanga kikmilifu kuabiliana na magendo nchini kote kwani ni
mojawapo wa mwanya mkubwa wa uvujaji wa mapato ya Serikali pamoja na
kukabiliana na vishoka na matapeli wanaochafua jina la TRA kusababisha
upotevu wa mapato au kushindwa kukusanya kwa wakati.
Amefafanua
kuwa katika kufikia malengo ya makusanyo wanaendeleza maandalizi ya
Bahati Nasibu kubwa ya EFD baada ya kukamilika kwa majaribio ya sasa
yanayoendelea Mkoa wa Kikodi Tegeta ili kuhamasisha utoaji na kudai
risiti za EFD.
Mambo mengine ni kuongeza kasi
ya utoaji elimu ya kodi kwa makundi mbalimbali pamoja kuhamasisha
ulipaji wa kodi kwa njia za ubunifu na shirikishi ikiwemo elimu ya
mlango kwa mlango, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, machapisho,
nyimbo mbalimbali za sanaa pamoja na kuweka mazingira ya kuaminiana kati
ya TRA na walipakodi.
Pia amesema mabadiliko
yaliyotokea yanagusa sekta mbali na sheria mbalimbali na sheria
mbalimbali za kodi ikiwemo Sheria ya Ushuru wa bidha sura ya 147, sheria
ya magari ya kigeni, sura ya 84, sheria ya kodi ya mapato, sura 332
sheria ya kodi ya ongezeko la thamani, sura 148 na sheria yamadini,
sura 123.
Nyingine ni Sheria ya Usafirishaji
Bidhaa Nje ya Nchi, Sura 196, Sheria ya Posta na Mawasiliano ya
Kielektroniki, Sura 306, Sheria ya Usiamaizi wa Forodha ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki ya mwaka 2004 na Sheria nyingine za mapato yasiyo ya
kodi.
Aidha amesema katika mabadiliko ya
sheria ya usimamizi wa kodi ambapo sheria ya sasa inamtaka kila
mwananchi mwanye Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kusajilwa na
kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kumwezesha kwenye
shughuli zake za kia siku.
Katika hatua
nyinginge, amesema mafaniko ya mwaka jana wa fedha 2020/21 yaltokana na
kuzingatia maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo ikiwemo
kukusanya kodi kwa weledi, kukaa na walipa kodi kutatua chanagmoto zao
ikiwa kuweka mazingira rafiki ya kulpa kodi zao pamoja na kuongeza kasi
ya kup0anua wigo wa kusajili walipakodi wapya.
Nyingine
ni kuwekeza kwenye Teknolojia ya Habari ya Mawasiliano (TEHAMA) na
uanzishwaji wa ritani za VAT kielektroniki ambao umeongeza ufanisi na
kuondoa mapungufu na udanganyifu pamoja na utoaji wa elimu na kuhamsisha
ulipaji kodi kwa hiari.
Kayombo amesema TRA
inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuiongezea watumishi 2,100 ili
kuongeza nguvu kazi ya pamoja na rasilimali mbalimbali.
No comments:
Post a Comment