HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2022

YANGA PRINCESS: TUTAWAPIGA KAMA NGOMA



Na Mwandishi Wetu

Wakati joto la Ligi Kuu Soka la Wanawake Tanzania Bara msimu wa 2022/2023 likizidi kupanda kikosi cha Yanga Princess kimeendelea kujinoa kwa ajili ya mapambano ya msimu ujao.

Katika kuimarisha kikosi hicho ambacho kimekuwa na usajili Mkubwa sana wa maingizo mapya ya nyota wa kigeni Leo wamecheza mechi ya kirafiki dhidi ya JMK Park Queens na kuwachakaza mabao (6-0)

Mabao ya Yanga Princess yamewekwa kambani na Grace bao moja, Precious mabao 2, Wincate mabao 2 na Blessing bao moja.

Mabinti hao wa Twiga na Jangwani Wana kibarua kizito cha kufuta Umalkia wa watani wao wa Jadi Simba Queens ambao wamelitawala Soka la Wanawake kwa misimu minne sasa.

Yganga Princess hawajawahi kutwaa ubingwa wa Ligi'Kuu Soka la Wanawake tangu kuanzoshwa kwake jambo ambalo limewapelekea kufanya usajili wa maana Ili kuwa na misuli ya kulisaka taji hilo msimu ujao.

Baada ya mchezo huo WA kirafiki Yanga Princess kupitia ukurasa wao wa Instagram wametoa kauli ya kuwa watawapiga kama ngoma wapinzani wao msimu ujao.


No comments:

Post a Comment

Pages