Na Mwandishi Wetu
Wakati joto la kuelekea mchezo wa marejeano kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) katika ya Al Hilal ya Sudan dhidi ya Yanga SC likiwa juuu Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe anena na wachambuzi.
Ally amesema kila mtu ana haki ya kutoa maoni na maoni ya mtu yanaheshimiwa, hiyo ni kutokana na kuwepo maneno mengi ya kutokuwapa nafasi ya Wananchi kusonga mbele kutokana na matokeo waliyoyapata katika mchezo wa kwanza hapa Dar es Salaam.
Yanga ililazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Al Hilal katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na sasa jumapili hii watakuwa na kazi ya kufanya mjini Khartoum nchini Sudan kutafuta matokeo waweze kusonga mbele.
"Kila mchambuzi ambaye anafanya kazi kwenye chombo cha habari ambacho anafanya kazi anaaminika, hayupo kwa bahati mbaya."
"Yanga hatuwezi kuingilia maoni yake, maoni yanatolewa sehemu yoyote duniani" "Kama wanaamini Yanga hawezi kufanya vizuri Khartoum, tunaheshimu maoni yao, sisi tunaamini kwenye mchezo wa mpira wa miguu." Ameongeza kuwa.
"Hatuwezi kujibizananao, kazi yetu ni kucheza mpira" "Wanaosema timu yetu haiwezi kufuzu, tukifuzu watakuwa upande wetu na wataelezea kitaalam kwa nini tumefuzu.
"Kwa hiyo tunaheshimu mawazo yao na tunaomba waendelee kuizungumza timu yetu ili tupate mahali pa kuboresha kutoka kwenye maoni wanayotoa" amesema..
"Hatupo hapa kumzuia mwandishi/mchambuzi yeyote kuizungumzia Yanga, tupo hapa kushirikiana na vyombo vya habari na wachambuzi kuhakikisha Yanga inakuwa brand kubwa Afrika" amebainisha Ally Kamwe.
Hata hivyo kuelekea mchezo huo Yanga wanatarajiwa kuondoka afajiri ya kesho kuelekea Sudan ambako mchezo huo utapigwa siku ya jumapili saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment