Na Mwandishi Wetu
Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Mtibwa Sugar ya Manungu Mkoani Morogoro kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara utakaochezwa saa 16:00 jioni.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, inayonolewa na Kocha Mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi ya mwisho na kwamba ipo tayari kwa mtanange huo ambao kimsingi utakuwa naushindani mkubwa.
Katika mchezo huo KMC FC itakuwa nyumbani kwa mara nyingine tena ambao pamoja na ushindani uliopo imejiandaa kuhakikisha kwamba kama Timu inapata ushindi muhimu hapo kesho.
" Tunakwenda kwenye mchezo mwingine tukiwa nyumbani, tunawaheshimu wapinzani wetu Mtibwa Sugar kwa kuwa ni Timu nzuri na wao pia wanahitaji matokeo, lakini pamoja na hayo kama Manispaa ya Kinondoni tumejipanga kupata ushindi licha ya kwamba katika mchezo uliopita tulipata sare hapa nyumbani.
"Tuna amini kuwa matokeo mazuri tutayapata kutokana na kwamba KMC FC tunawachezaji wazuri na wenye ubora mkubwa ambao wanaweza kupambana kutafuta matokeo, na siku zote Timu Bora huwa haitoki sare mara mbili kwenye uwanja wa nyumbani."
"Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wako vizuri isipokuwa Ibrahimu Ame, Emmanuel Mvuyekure pamoja na Kelvin Kijili ambao wanachangamoto ya majeraha waliyoyapata wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni uliochezwa siku ya Jumanne ya Oktoba 11 na kumalizika kwa sare ya bila kufungana."
Amebainisha kuwa wachezaji walio salia wanalojukumu la kuhakikisha timu inapata matokeo.
"Hata hivyo mbali na wachezaji hao kuwa na changamoto ya majeraha, lakini wachezaji wengine wana hari na morali nzuri , kikubwa mashabiki, wana Kinondoni kesho wajitokeze kwa wingi kutoa sapoti kwa vijana wetu ambao wanaenda kupambania alama tatu muhimu."
October 14, 2022
Home
Unlabelled
KMC FC KUWAKARIBISHA MTIBWA SUGAR KESHO UWANJA WA UHURU
KMC FC KUWAKARIBISHA MTIBWA SUGAR KESHO UWANJA WA UHURU
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment