Na Mwandishi Wetu
NYOTA wa Klabu ya Yanga SC Gael Bigirimana amewaomba mashabiki wa Klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Yanga watashuka kwenye Dimba la Benjamin Mkapa kuwkaribisha Al Hilal katika mchezo wa kwanza hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kuwania kufuzu hatua ya makundi kabla ya kurejeana nao mjini Khatoum wiki moja ijayo.
Akizungumza na wandishi wa Habari mchana wa leo Bigirimana amesema kama wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na wako tayari kupambana na Al Hilal hapo kesho.
"Kama Wachezaji tunafahamu umuhimu wa mchezo huu, tunafahamu una maana gani kwa klabu na mashabiki. Jambo kubwa na la muhimu kwentu ni kuhakikisha kuwa tunaenda kushinda huu mchezo"
"Kutokana na uzoefu wa baadhi yetu ndani ya kikosi tunahimizana jinsi ya kuiwezesha timu iweze kufikia malengo, tumewatazama wapinzani wetu na tumejua uimara wao na madhaifu yao hivyo tupo tayari." Amesema na kuongeza kuwa.
"Kwa kutambua umuhimu wa mashabiki wetu nawaomba sana wajitokeze kwa wingi waujaze uwanja na kushangilia muda wote wa mchezo na kazi ya matokeo watuachie sisi tutawapatia"
"Natambua tuna mashabiki bora hivyo waje waonyeshe ubora wao katika mchezo mkubwa ambao wao ni muhimu kuwepo" amesema Bigirimana.
Mwisho wa mchezo na kazi ya matokeo watuachie sisi tutawapatia"
"Natambua tuna mashabiki bora hivyo waje waonyeshe ubora wao katika mchezo mkubwa ambao wao ni muhimu kuwepo" amesema Bigir 21imana.
No comments:
Post a Comment