Wakati
makampuni na taasisi dunia nzima zikiadhimisha ‘Wiki ya Huduma kwa
Wateja’ mwaka 2022, Benki ya CRDB imeianza wiki hiyo kwa kuwashukuru
wateja wake kwa maoni na ushauri ambao umeiwezesha benki hiyo kutoa
huduma bora na zenye viwango vya kimataifa kwa jamii.
Salamu
hizo za shukrani zimetolewa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB,
Fredrick Nshekanabo wakati wa hafla iliyofanyika katika tawi la Benki
hiyo lililopo Oysterbay, Jijini Dar es Salaam. Nshekanabo alisema wateja
wamekuwa msingi mkubwa kwa Benki ya CRDB kufikia mafanikio ambayo
imekuwa ikiyapata kufikia kuwa ‘Benki Bora zaidi Tanzania’.
“Tukiongozwa
na kaulimbiu yetu ya ‘Benki inayomsikiliza mteja’ tumekuwa tukipokea
maoni na ushauri wa wateja ambao kwa kiasi kikubwa umechangia ubora wa
huduma na bidhaa zinazotolewa na benki yetu. Hii inaonyesha ni kwanamna
gani mteja amepewa kipaumbele kikubwa katika mkakati wa biashara yetu,”
aliongezea Nshekanabo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB,
Yolanda Uriyo amesema pamoja na kuwashukuru wateja, katika Wiki ya
Huduma kwa Wateja mwaka huu wamedhamiria kuwasherekea wale wote walio
mstari wa mbele kuiwezesha benki hiyo kutoa huduma bora”.
“Wakati
dunia nzima ikiadhimisha wiki hii kwa kaulimbiu ya ‘Celebrate Service’
inayomaanisha kusherehekea huduma, kwetu sisi hii ni zaidi ya kaulimbiu
kwani mafanikio tuliyonayo yanatulazimisha kuwasherehekea wanaotufanya
tuwe bora zaidi; wateja na wafanyakazi wetu,” alifafanua Uriyo.
Uriyo
alisema Benki ya CRDB itaitumia wiki hii kuwashkuru na kuwasherehekea
wateja ambao wamekuwa chachu ya huduma bora zinazotolewa na benki hiyo.
Aidha, watakuwa wakiwasherekea wafanyakazi ambao wamekuwa wakitoa huduma
bora kwa weledi na ubunifu mkubwa.
Benki
ya CRDB inatajwa kuwa benki inayoongoza kwa huduma bora kwa wateja.
Mwaka huu benki hiyo imetunukiwa tuzo ya ‘Benki Bora Tanzania’ na jarida
maarufu duniani la nchini Uingereza la Euromoney. Mwaka jana mwishoni
benki hiyo ilitunukiwa ‘Tuzo ya Ubora’ na Taasisi ya Utafiti wa Ubora
barani Ulaya (European Society for Quality Research).
Katika
miaka ya hivi karibuni Benki ya CRDB imeweka kipaumbele na kufanya
uwekezaji mkubwa katika huduma kwa wateja. Benki hiyo imewekeza katika
mifumo ya kisasa na ya kidijitali ya utoaji huduma, ikiwamo mifumo ya
mawasiliano, ambayo imesaidia kuongeza ufanisi katika matawi yake zaidi
ya 260 yaliyosambaa kote nchini.
Uwekezaji
huu pia umeongeza ufanisi katika njia mbadala za utoaji huduma; CRDB
Wakala zaidi ya 22,000, ATMs zaidi ya 550, na huduma za SimBanking,
SimAccount, na Internet banking. “Benki pia imewekeza katika mafunzo kwa
wafanyakazi ili kuwawezesha kupata weledi pindi wanapowahudumia wateja.
Hii imeenda sambamba na uboreshaji wa taratibu zetu za utoaji huduma
(processes) ili ziendane na mahitaji ya wateja,” alisema Afisa Mkuu wa
Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kauli
mbiu "Sherehekea Huduma" iliyofanyika leo kwenye Tawi la Benki ya CRDB,
Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni (wa pili kulia) akikabidhi zawadi mmoja wa
wateja wa benki ya CRDB, Dk. Redempta Mbatia (kushoto) wakati wa hafla
ya ufunguzi rasmi wa wiki ya huduma kwa wateja yenye kauli mbiu 'Sherehe
Huduma' iliyofanyika leo katika Tawi la Ostabey Masaki jijini Dar es
Salaam (wa pili kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick
Nshekanabo na kulia ni Mkuu wa Kitengo Cha Huduma kwa Wateja wa benki ya
CRDB, Yolanda Uriyo.
Afisa
Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick
Nshekanabo, akizungumza na wateja wa benki hiyo katika hafla ya uzinduzi
wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika katika Tawi la Oyster bay Masaki jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Kitengo Cha Huduma kwa Wateja wa benki ya
CRDB, Yolanda Uriyo, na wateja wa Benki ya CRDB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Baadhi
wa Wateja wa Benki ya CRDB wakishiriki shidano fupi la kupamba Keki
ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja
yenye kauli
mbiu "Sherehekea Huduma" iliyofanyika leo kwenye Tawi la Benki ya CRDB,
Oysterbay, jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (wa pili kulia) akimkabidhi
zawadi ya Shampeni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline
Kamuhanda baada ya kushiriki shidano fupi la kupamba Keki ikiwa ni
sehemu ya kusherehekea ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kauli
mbiu "Sherehekea Huduma" iliyofanyika leo kwenye Tawi la Benki ya CRDB,
Oysterbay, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Afisa Mkuu wa Fedha
wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo (wapili kushoto) pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo.
Sehemu ya wateja wa wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment