NA MWANDISHI WETU
Mamlaka ya Masoko Ya Mitaji na Dhamana (CMSA), imezindua wiki ya uwekezaji duniani.
CMSA
kwa kushirikia na Taasisi ya Kimataifa inayohusika na Usimamizi na
watoaji wa viwango vya Kimataifa vya masoko ya mitaji ulimwenguni
(IOSCO) inashiriki katika kuadhimisha wiki ya wawekezaji ulimwenguni
iliyoanza Oktoba 3 mpaka Oktoba 7, 2022.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA, Nicodemus Mkama, katika taarifa yake
amesema lengo la kushiriki Wiki ya Wawekezaji Duniani ni kuongeza uelewa
kuhusu umuhimu wa elimu kwa umma na ulinzi wa maslahi ya wawekezaji kwa
kuangazia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka za usimamizi wa
masoko ya mitaji katika maeneo haya muhimu.
"Wiki
ya Wawekezaji Ulimwenguni inahusisha Mamlaka za usimamizi wa masoko ya
mitaji ambazo ziko chini ya IOSCO pamoja na wanachama wengine wa IOSCO
katika mabara sita ambazo hufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na
uzinduzi wa njia za mawasiliano na huduma zinazomlenga mteja, kukuza
ushindani wenye tija unaolenga kuongeza wigo wa mikakati mbalimbali ya
utoaji wa elimu ya wawekezaji,"amesema.
Pia wataandaa warsha na makongamano, pamoja na kutumia Mamlaka zao kuendesha kampeni za kitaifa.
Mkama
amesema Wiki ya wawekezaji inatoa nafasi ya upendeleo maalumu kwa
wanachama wa IOSCO kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wote wanaotoa
elimu ya uwekezaji kwa umma kwa ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni uhimilivu wa wawekezaji na Mitaji Endelevu.
Mkama
amesema Wiki ya Wawekezaji Ulimwenguni inatarajiwa kuongeza uelewa wa
fursa na faida za kutumia masoko ya mitaji nchini ambao unalenga “
Kutambua Ushindani na Maendeleo ya Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”.
Pia
inalenga kuongeza ushiriki wa wawekezaji katika masoko ya mitaji hivyo
kuwezesha utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha
na Mpango Mkuu wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha.
Aidha
amesema wiki ya Wawekezaji Ulimwenguni imeambatana na maono ya Serikali
ya awamu ya sita chini ya uongozi uliotukuka wa Rais Samia Suluhu
Hassan, ambao unalenga kuweka mazingira wezeshi kwa maendeleo ya sekta
ya fedha kwa kuchochea maendeleo na ukuaji wa uchumi Nchini.
Katika
kuadhimisha wiki hii, CMSA itafanya shughuli mbalimbali zinazolenga
kuongeza uelewa, upatikanaji, ushiriki na kulinda maslahi ya mwekezaji
katika masoko ya mitaji kuanzia tarehe 3 mpaka 7 Oktoba 2022.
Programu
hii inalenga kuimarisha uelewa kuhusu masoko ya mitaji hivyo kuchangia
kwenye ajenda ya Taifa ya kuboresha Huduma Jumuishi za kifedha na
maendeleo ya uchumi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment