HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 09, 2022

DE AGOSTO WAKUBALI YAISHE KWA MNYAMA


Na Mwandishi Wetu


Fantastic, yes it was fantastic for Simba SC, wanachokifanya Simba kimataifa hata kama hujui kiingereza utafurahi tu.

Mechi ngumu huchezwa kigumu na akili kubwa, unaweza sema wanakutana na wapinzani wepesi lakini itazame Simba wanavyocheza wakiwa Ligi ya Mabingwa Afrika utaelewa wamekomaa kila eneo japo mapungufu yapo lakini ni ngumu kuzima roho zao ngumu huku.

Ulikuwa mchezo wenye ushindani kwa pande zote mbili lakini hesabu za Juma Mgunda ni kuicheza mechi kimkakati, pata bao mapema kisha miliki mpira wape mpira. Ndicho lilionekana dakika 45 za kwanza.

Chama ni kama mishipa ya damu kwenye Moyo ndani Simba, huamua mapigo yaende kasi ama taratibu, utulivu wake ni zaidi ya kasi ya Hussein Bolt, alifunga kabla ya kufunga alivyowahadaa walinzi wa De Agosto.

De Agosto walijaribu kupeleka presha kwenye lango la Simba kupitia pembeni lakini zao lao la mwisho lilikuwa linaishia kwa Onyanga na Inonga ama Mzamiru na Kanoute.

Simba walikuwa bora sana jinsi walivyokuwa wanafanya shinikizo katika kuutafuta mpira, hapa ndio ubora wa wachezaji wote ulikuwa mtaji wa Simba kuwazima De Agosto.

Kipindi cha pili De Agosto ni kama walitiwa ndimu na kulazimisha mashambulizi huku viungo wao wa ulinzi wakiacha nafasi kubwa na walinzi wao na mawinga wakawa hawawasaidii walinzi wa pembeni wanapopotez mipira.

Chama na Phiri walizama kwenye hayo mashimo kulia na kushoto mabao mawili yakapatikana kupitia kwa Mwenda na Phiri.

Jenerali Moses Phiri anachojia ni kufunga na kufunga kuko damuni mwake anatumia vema pasi ya Chama na kuipatia Simba bao la tatu na la ushindi.

De Agosto walikuwa hawana namna kwa sababu walitaka kutumia mipira ya juu lakini shinikizo la Simba lilikuwa linaua mipango yao na kukosa makali.

Licha ya ubora wa mchezaji mmoja mmoja kushindwa kuwapa walichohitaji iliwallpa kwa kupata mkwaju wa penati na kuweza kupata  bao la kufutia machozi.

Mzamiru Yassin ni ngumu kumpenda kama hupendi mpira ila mapafu yake ndio silaha ya Simba katika kujilinda na kushambulia.

De Agosto wanahitaji kushinda mabao 4-0 mchezo wa marejeano katika Dimba la Benjamin Mkapa wiki ijayo, swali ni je wataweza kuupanda mlima huo ni jambo la kusubiri na kuona.

Kocha Juma Mgunda ni swali gani hajajibu ndani ya mechi Saba ameruhusu bao moja kwa mkwaju wa penati.

Ni dakika 90 za ugenini zilizolibeba jina la Simba kwenye bendera ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

No comments:

Post a Comment

Pages