HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 09, 2022

Nape awataka watoa huduma wote nchini kutumia mfumo wa anuani za makazi

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.


Na Mwandishi wetu


Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

amewataka watoa huduma wote nchini kutumia mfumo wa anuani za makazi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi nchini.


Nape ameyasema hayo leo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Umoja wa Posta Duniani (UPU) yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC).


Amesema ni muhimu kwa watoa huduma wote nchini kutumia mfumo huo wa anuani za makazi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.


"Na hapa niwashukuru sana Shirika la Posta Tanzania (TPC), kama kuna taasisi ambayo imeshiriki vizuri sana kuhakikisha mfumo wa anuani za makazi unakaa mahali pake ni shirika hili la Posta, tunapaswa kuwapongeza,"  amesema Nape


Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan  imejipanga kuwawezesha watoa huduma za posta ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi bila kulazimika kufika kwenye ofisi za posta.


"Hilo litawezekana kwa kuwa serikali inakamilisha utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi ambao ni miundombinu muhimu katika utekelezaji wa huduma za posta hasa katika kumfikishia mteja barua au mzigo katika eneo lake la makazi," amesema


Aidha amesema takwimu za Tanzania zinaonesha kuwa simu ambazo zipo mtaani kwa sasa ni Milioni 58 lakini kati ya hizo, milioni 37 wanatumia simu kama njia yao ya kufanya manunuzi.


"Kwa takwimu hizo ni wazi kuwa watanzania wengi wanatumia simu na Posta wanasema wapo kiganjani hivyo wakiweza kiwatumia watu hapo Milioni 37 ni mtaji wao mkubwa sana," amesema


Kwa upande wake Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo amesema Posta ya sasa ni ya kila mtanzania kwani katika eneo la usalama wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudhibiti usafirishaji haramu wa silaha za kivita.


"Tunashirikiana na vyombo vya usalama katika kudhibiti mtandao wa usafirishaji wa dawa za kulevya, na ikitokea watu wanajaribu kufanya uhalifu huo kwa namna ambavyo tumejipanga, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria," amesema


Hata hivyo amesema pia Posta wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia duka mtandao kwa kutoa fursa kwa watanzania ambao ni wafanyabiashara kuuza na kuunua bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kupitia duka hilo.


"Katika eneo la elimu, tunashirikiana kwa ukaribu na Baraza la Mitihani (NECTA) na Bodi ya Mikopo katika kuwasaidia wanafunzi wanapofanya usajili wa kufanya mambo yao kisha kuyasafirisha kwa njia ya Posta," Mbodo na kuongeza


"Pia tunashirikiana na Wizara ya Afya katika kusafirisha sampuli za maabara zote nchini kutoka kwenye vituo vya afya ngazi ya kwanza kwenda vituo vya afya ngazi ya pili na kisha kwenda kwenye maabara za uchunguzi na baadae kùrejesha majibu, kupitia mfumo huo tumeajiri zaidi ya vijana 500 wa bodaboda," amesema a

No comments:

Post a Comment

Pages