Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabani, Wlbroad Mutafungwa.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jeshi
la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini limewataka madareva
Wanaofanya kazi Serikalini kuzingatia sheria za barabarani nakuacha
tabia ya kudhani kuwa wapo juu ya sheria kwani wamekuwa wakisababisha
ajali.
Hayo
yamesemwa jijini humo na Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani
Nchini, Wilbroad Mutafungwa wakati wa Mafunzo ya siku moja Kwa Madereva
wa Serikali yenye lengo la kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao Kwa
kuzingatia sheria za Barabarani Ili kupunguza ajali zinazojitokeza
nakusababisha vifo na ulemevu wa kudumu.
"Ninyi
Madereva mnafanya kazi bila kuzingatia sheria japokuwa mmepata Mafunzo
kutoka katika vyuo vya usafirishaji vinavyotambulika
kisheria,mmetahiniwa na kukabidhiwa chombo cha moto Kwa mujibu wa
sheria,lakini mmekuwa ni sehemu ya kusababisha ajari kutokana na kuzalau
sheria za Barabarani nakujiona nyinyi mpo juu ya sheria" amesema
Mutafungwa
Amebainisha
kuwa asilimia 90 ya ajali zinazojitokeza zimekuwa zikisababishwa na
tabia za madereva hao kitokuzingatia sheria za barabarani huku asilimia
zingine za ajali zikisababishwa na masuala ya miundombinu ya barabara na
sababu zingine.
Mutafungwa
amesisitiza katika kipindi cha mwezi January 2022 hadi Agosti 2022
ajali zilikuwa 1,177 katika hizo ajali zilizotokana magari ya serikali
135 sawa na asilimia 11.5 huku jumla ya vifo vyote 11038 na 90
vilitokana na magari ya serikali sawa na asilimia 8 .7
Sambamba
na hayo amesema Majeruhi wote wa ajali walikuwa 1,556 walitokana na
magari ya serikali 211 sawa na asilimia 13 .6 hivyo ajali ya magari ya
serikali umekuwa siyo jambo la kustua imekuwa kawaida kwani asilimia
kubwa hujisababishia wenyewe kutokana na viongozi kuwafanya Madereva wao
wawe juu ya sheria hawaonywi.
No comments:
Post a Comment