Na WAJJWM, Dar es salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali haitavumilia vitendo vya ukatili vinavyoendelea kutokea kwenye jamii.
Waziri
Gwajima ameyasema hayo tarehe 07 Oktoba, akiwa katika ziara yake Jijini
Dar es salaam, kata ya Kivule alipomtembelea Mtoto Daudi Mabwega mwenye
umri wa miaka minne aliyefanyiwa ukatili na baba yake mzazi wa kuchomwa
ya maji ya moto mkononi kwa kosa la kula mboga bila idhini ya mzazi
huyo.
Amesema
Jamii inatakiwa kuwatunza watoto kwani ni hazina kwa Taifa hivyo
wanapaswa kulindwa kwa hali yoyote na akiwa ni Waziri mwenye dhamana ya
watoto atahakikisha haki zao zinalindwa.
"Mzazi
ni mtu wa kwanza anayetakiwa kuwa Faraja kwa Mtoto wake aliyemzaa,
hatuwezi kuendelea kuvumilia kuona Wazazi ambao badala ya kuwa viongozi
wanawakatili hawa watoto, Serikali itamfikia kila mzazi, mlezi na
mwanajamii aliyefanya ukatili kwa mwanajamii mwingine hususani watoto"
amesema Mhe. Gwajima.
Kwa
upande wake Afisa Utawi wa Jamii, hospitali ya Wilaya ya Kivule Irene
Shembelu aliyeibua ukatili huo amesema Mtoto huyo alifanyiwa ukatili na
baba yake baada ya migogoro ya kifamilia iliyosababisha mama wa mtoto
kuondoka na kuwaacha watoto na baba yao pekee.
"Tuliipokea
kesi ya Mtoto huyu kuwa amekatiliwa na baba yake mzazi kwa kosa la kula
maharage waliyotegemea kula baada ya baba kurudi, kwani watoto hawa
wanajilea wenyewe, baba akitoa asubuhi anarudi usiku" Alisema Irene
Shembelu.
Kwa
upande wake Inspekta Mdasi Lukato akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Dawati la Jinsia Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam amesema hatua kali
zitachukuliwa kwa kitendo kilichofanyika na baba huyo.
Naye
mlezi aliyeaminiwa kumlea Mtoto Daudi na ndugu zake Bi. Zahra Omary
(fit person) amesema alimpokea Mtoto huyo mwezi Agosti mwaka huu kutoka
kwa Afisa Ustawi wa Jamii akiwa na Hali mbaya.
Baadhi
ya wananchi wakizungumza katika mkutano wa hadhara wamemshukuru Mhe.
Gwajima kwa kuwatembelea na kujua changamoto zao kwani vitendo vya
ukatili katika kata hiyo ni vingi lakini wanajamii wanakabiliana navyo
kwa jitihada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment