Malkia wa
Uholanzi, Malkia Maxima amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea mkoani
Kilimanjaro ambapo alianzia ziara yake jana tarehe 17 Oktoba 2022 baada
ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 17 –
19 Oktoba, 2022.
Mara
baada ya Malkia Maxima kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam, alipokelewa na Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza.
Malkia
Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo
anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Oktoba 2022.
Mbali
na kukutana na Mhe. Rais Samia pia Malkia Maxima kabla ya kuhitimisha
ziara yake hapa nchini, anatarajia pia kukutana na viongozi mbalimbali
waandamizi wa Serikali.
|
Malkia
wa Uholanzi, Malkia Maxima akipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es
Salaam |
|
Malkia
wa Uholanzi, Malkia Maxima akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake
mwenye suti ya kijivu ni Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza |
|
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza akiteta jambo
na Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima baada
ya Malkia kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam |
|
Malkia
wa Uholanzi, Malkia Maxima akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es
Salaam |
No comments:
Post a Comment