MSIMU
wa tatu wa Tamasha kubwa la Marafiki Music Festival umewadia ambapo
kivumbi kizito cha burudani kinatazamiwa kuanza kutimka Alhamisi hii
ndani ya Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam kwa mtonyo mdogo wa buku
15 tu.
Bosi wa Kampuni ya Asedeva
ambao ndio waandaaji, Isack Abeneko, amesema bendi 20 pamoja na zaidi ya
wasanii 128 kutoka mataifa mbalimbali Afrika, wakiwamo Man Fongo na
Balaa MC kwa hapa nchini, wanatarajiwa kupamba shughuli hiyo.
"Tamasha
la mwaka huu litakuwa ni la siku nne ambapo kuanzia Oktoba 6 hadi 8,
litarindima hapa Dar es Salaam kabla ya Oktoba 9 kufunga dimba kwenye
ukumbi wa Firefly, Bagamoyo, Pwani," amesema Abeneko na kuongeza:
"Viingilio
kwenye shughuli hiyo vitakuwa ni sh 15,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa
wanafunzi watakaokuwa na vitambulisho vya shule, lakini pia tiketi za
awali tayari zimeshaanza kuuzwa kwa bei ya sh 20,000 kwa shoo zote nne
na 10,000 kwa tukio moja."
No comments:
Post a Comment