Na Mwandishi Wetu
Ubora ni neno linalojitosheleza kuelezea kilicho bora, Ndivyo ambavyo Simba SC wanaonyesha ubora kwa kushusha kipigo kizito kwa Mtibwa Sugar cha mabao (5-0).
Ilikuwa mchezo mgumu zaidi kwa Mtibwa Sugar kwa namna ambavyo walikuja kupishana na Simba katika maeneo mengi ya Uwnaja jambo ambalo lilipelekea shughuli ya Simba kuwa nyepesi.
Mpango wa Mwalimu Salum Mayanga wa 4:4:2 , dhidi ya Juma Mgunda na 4:2:3:1, ambapo Simba walikuwa wanabadilika kuwa na wachezaji watano katika mwa uwanja kwa Ubora wao kazi ikaishia hapo.
Pascal Kitenge na Balama Mapinduzi walikuwa na kazi nzito sana kuwakabili viungo Mkude, Chama na Mzamiru katika ya dimba huku Pape Sakho akiwa nyuma yao, waliishia kucheza madhabi yaliyopekea kupata kadi mbili nyekundu.
Mabao ya Pape Sakho akifunga mara mbili Agustin Okrah, Moses Phiri na Mzamiru Yassin yametosha kuwa sambalatisha Mtibwa Sugar.
Kwa ushindi huo Simba wanakwea hadi nafasi ya pili wakifikisha pointi 17 nyuka ya vinara Yanga wenye pointi 20.
No comments:
Post a Comment