Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Sara Mlaki, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo hawapo pichani iliyofanyika Wilayani Kibaha.
Na Victor Masangu, Pwani
Serikali
mkoani Pwani katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu
Hassan kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi za chini imejenga vituo
vya utayari vipatavyo 36 katika halmashauri zote lengo ikiwa ni
kuwapatia elimu watoto waliosahaulika kupata fursa ya elimu ngazi ya
awali.
Hayo
yamebainishwa na Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani wakati wa kufungua warsha
ya mpango maalumu kwa ajili ya kuwandaa watoto hao waweze kuandaliwa
vizuri katika elimu ya awali kabla awajajiunga na darasa la kwanza.
Aidha
afisa elimu huyo alibainisha kwamba nia yao kubwa katika mpango huo wa
utayari ni kuwajengea uwezo na mahalifa ya katika suala zima la kuweza
kujua kusoma,Kuhesabu na kuandika kabla ya kuingia darasa la kwanza.
Pia
aliongeza kuwa wameamua kuwakutanisha wadau mbali mbali wa elimu
wakiwemo madiwani,watendaji kata,waratibu elimu,wakuu wa shule ili
tuweze kuweka mpango wa kuboresha sekta ya elimu kwa watoto hao ambao
walishindwa kupata fursa ya kupata elimu ya awali.
"Lengo
letu ni kuanzisha vituo vya utayari katika halmashauri zetu tisa kwa
ajili ya watoto wetu wa kuanzia miaka 5 hadi 9 ili waweze kupata elimu
ya awali kabla ya kuanza kujiunga na darasa la kwanza na halmashauri
zetu zinatupa ushirikiano katika kufanikisha Jambo hili"alibainisha
Sara.
Kadhalika alisema
kuwa mpango huo ambao umeanzishwa na serikali utawasaidia watoto ambao
wamekosa fursa ya kupata elimu kuweza kujifunza zaidi katika
kusoma,kuhesabu na kuandika.
Kwa
upande wake afisa elimu ya watu wazima katika halmashauri ya Wilaya ya
Rufiji Hamisi Chikaula amebainisha mpango huo wa utayari wa kuanzia
vituo utaweza kuwa mkombozi mkubwa wa kuwasaidia watoto kupata elimu
iliyo bora kuanzia ngazi za chini.
Chikaula
ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wawezeshaji katika Warsha hiyo aliongeza
kuwa katika mpango huo kila halmashauri inajenga vituo vinne ambavyo
vitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa watoto kupata elimu ya awali.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya mkuza Focus Bundala ambaye ameshiriki
katika Warsha hiyo ameahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote ambayo
wameyapata katika suala zima la kuwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka
watoto wao katika vituo hivyo.
Diwani
wa kata ya Visiga Kambi Legeza aliipongeza serikali ya awamu ya sita
kwa kuanzisha mpango huo wa kujenga vituo ambavyo vitatumika katika
kuwasaidia watoto ambao walikosa nafasi katika elimu ya awali.
Caption-
1 Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani Sara Mlaki akizungumza na washiriki wa
warsha hiyo hawapo pichani iliyofanyika Wilayani Kibaha.
Caption-2 Baadhi ya washiriki waliohudhulia katika warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment