HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 28, 2022

SIMBA SC, MO ASSURANCE KULINDA AFYA ZA WACHEZAJI, WATENDAJI

Na John Richard Marwa


Klabu ya Simba imeingia mkataba wa miaka miwili wa bima ya afya kwa wachezaji, benchi la ufundi na menejimenti ya Simba na Kampuni ya bima ya Mo Assurance wenye thamani ya Tsh million 250.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amesema lengo ni kuhakikisha wafanyakazi wote wanakuwa na bima ya afya.

"Lengo kuu ni kuhakikisha wafanyakazi wote wanakuwa na bima ya afya. Leo tunaingia mkataba wa bima na Mo Assurance, watakuwa wanatoa bima kwa wachezaji wote, benchi la ufundi na menejimenti. Lakini pia hakuna gharama yoyote kwa upande wa Simba. Kama Simba tunajivunia sana."- CEO Barbara Gonzalez.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa masoko wa Me TL Group Fatema Dewji amesema.

"Wote tunafahamu katika maisha ya mwanadamu afya ni muhimu sana, kwa kutambua hilo Mo Assurance imekuja na habari njema kwa wachezaji wote wa Simba, benchi la ufundi, menejimenti pamoja na familia zao."

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Mo Assurance, Gregory Fortes amesema wameamua kufanya hivyo Ili kutoa uhuru kwa watendaji wote wa Simba kuwa na wakati mzuri wa kutekeleza majukumu yao.



"Sisi kama kampuni tumeamua kutoa bima ya afya, kuna aina tofauti kama watu wanaolazwa, wanaokwenda kutibiwa na kurudi nyumbani na mambo mengine madogo madogo kama matatizo ya meno, macho lakini pia tumeongeza huduma ya majeraha yanayotokana na michezo."- CEO wa Mo Assurance, Gregory Fortes.

Wakati huo Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema.


"Ili upate ufanisi wa mtu kwenye kufanya kazi ni lazima awe huru kwenye malazi, yeye mwenyewe kuugua au watu wanaomzunguka. Sasa ili kuwafanya wafanyakazi wa Simba kuwa kwenye ufanisi wao, leo tumewaletea bima ya kushughulika na afya zao."- Ahmed Ally.

No comments:

Post a Comment

Pages