HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 06, 2022

TEMBO WORRIES YAONDOSHWA NA HAITI KWA MBINDE



Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Taifa Soka la Watu wenye ulemavu Tembo Worries imeshindwa kufua dafu mbele ya wababe Timu ya Taifa y Haiti mchezo wa Robo Fainali Kwa mabao (4-1).

Haiti waliingia kwenye mchezo huo kwa kasi na kuandika mabao ya haraka haraka kiasi cha Tembo kushindwa kuhimili hiyo presha.

Hadi kipindi cha kwanza kinahitimika Haiti (3-1) Tembo Worries. Kipindi cha pili Haiti walipigilia msumari wa mwisho na hadi kipyenga cha mwisho Haiti (4-1) Tembo Worries.

Kwa matokeo hayo Tembo Worries wameondoshwa kwenye mbio za kusaka Bingwa wa Fainali hizo zinazoendelea nchini Uturuki.

Licha ya kushindwa kutinga Nusu Fainali Tembo Worries bado wataendelea kusalia nchini Uturuki kutafuta ubora wa viwango vya Dunia kuanzia namba moja hadi nane.

Kwa mujibu wa kanuni timu zote zilizotinga hatua ya Robo Fainali ama nane Bora zinaendelea kuwa kwenye kituo cha mashindano kutafuta viwango vya ubora.


Ikumbukwe kuwa Tembo Worries katika hatua ya Robo 16 Bora  baada ya kuwachakaza Japan (3-1). Mchezo WA hatua ya 16 Bora ulipigwa jioni ya leo huko nchini Uturuki.

Ulikuwa ushindi wa pili mtawalia kwa Tembo Worries kushinda katika fainali hizo ikiwa ni baada ya kuwachakaza Uzbekistan katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi.

Haya ni mafanikio makubwa zaidi kwa timu za Taifa hasa kwa Tanzania kuwa na uwakilishi Bora ikiwa ni mara ya kwanza kama Taifa limepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo makubwa Ulimwengu kwa watu wenye ulemavu.

Awali Tembo Warriors, ilitinga  16 Bora ya Fainali za Dunia za Soka la Walemavu baada ya kumaliza ikiwa na pointi nne katika  kundi lake ikiwa ya tatu nyuma ya Poland na Uzbekistan.

Tembo Warriors imekata tiketi hiyo baada ya kuwa moja ya timu nne zilizoshika nafasi ya tatu zikiwa na uwiano mzuri (best looser) baada ya kuifunga Uzbekistan, kutoka sare na Hispania na kufungwa na Poland.

Kila la heri Tembo Worries katika michuano hiyo mikubwa Watanzania wako nanyi katika kupeperusha bendera ya Jamhuri ya Wapambananji.

No comments:

Post a Comment

Pages