Mkutano ukiendelea.
Dk. Christina Mdingi akitoa mada kuhusu waandishi wa habari kuondosha dhana potofu juu ya chanjo ya Uviko-19.
Mwandishi mkongwe Yasin Sadiki akichangia mada.
Mjumbe Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri, Neville Meena akichangia mada.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Waandishi wa habari wametakiwa kuandika habari sahihi kuhusu chanjo ya Uviko-19 ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo.
Afisa Afya wa Mkoa wa Dar es Salaam Enezael Ayo amesema kuwa alipokuwa anawasilisha mada kwenye semina ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyoratibiwa na Shirika la Internews na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).
Amewasihi waandishi wa Habari kuiondosha dhana potofu inayokwamisha zoezi la chanjo ya ugonjwa huo kwenye jamii.
Enezael
amesema kuwa baadhi ya viongozi wa dini waliwahi kutoa taarifa
zilizopotosha umma juu ya chanjo hiyo ilhali chanjo hiyo ni salama.
"Waandishi
wa Habari mtusaidie kuondosha dhana potofu juu chanjo kwa sababu hakuna
mtu yoyote aliyepata madhara tangu chanjo hizi zilivyozinduliwa na Rais
Samia Suluhu Hassan" amesema Enezael.
Ameitaja
changamoto nyingine watu kujisahau baada ya kuona kiwango cha maambukizi
kushuka ambapo waliacha utaratibu wa kuchukua tahadhari ikiwa kuacha
kunawa mikono , kujisafisha kwa kitakasa mikono, kuvaa barakoa,
Amesema
kuwa tangu Tanzania kuingia kwenye hatua za kuchukua tahadhari za
ugonjwa huo maradhi mengi yamupungua kama vile kipindupindu.
Amezitaja
takwimu za watu waliochanja jijini Dar es Salaam ambapo tayari
washachanjwa ni zaidi ya watu Milioni mbili sawa na asimilia 85 huku
malengo yakiwa ni watu 3331079 .
Amesema kuwa wataalam wa Afya
walishirikiana na watoa huduma ngazi ya jamii, wenyekiti wa serikali za
mitaa kwa kufanya kazi ya kuhamasisha chanjo nyumba kwa nyumba pamoja na
hamasa ya waandishi wa habari.
Naye Dk. Christina Mdingi mtaalam
wa masuala ya afya ametoa msisitizo kwa waandishi wa habari kuwa mstari
wa mbele ili kuhakikisha kuwa wananchi wanabaki salama.
"Tuwajengee wananchi tabia ya kuamini na kutekeleza yale yanayohadharishwa na wataalam wetu wa afya"
"Wanahabari
wakikosea sentensi moja tu jamii imekwisha jamii inawaamini sana kwa
hiyo nyie watu muhimu kwenye hili" amesema Dk. Mdingi.
Nevile
Meena mhariri na mwandishi wa habari wa siku nyingi kwenye semina hiyo
amewaeleza waandishi wa habari namna bora ya kuzikabili taarifa za
upotoshaji .
Amesema kuwa changamoto kuwa kuhusu habari za chanjo ni uvumi, tetesi, nandhana potofu .
Amezitaja
baadhi ya dhana zilizoenea ni pamoja na kuhusishwa chanjo na ugonjwa
huo na biashara, watu waliochanjwa kugeuka mazombi, na chanjo zenye
majina tofauti .
Meena amesema kuwa kuliibuka taarifa nyingi za upotoshaji juu ya chanjo ya Uviko 19 pale siku chanjo hizo zilipofika nchini.
"Kazi
ya serikali inafanana na ile ya mzazi ya kuhakikisha watoto wake wapo
salama hivyo Rais hawezi kukubali wananchi wake wafe" amesema Meena.
Amesema kuwa waandishi wa habari wakifanya kazi zao vizuri wataondosha dhana potofu iliyojengwa kwa umma.
No comments:
Post a Comment