Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akitoa hotuba yake wakati wa kufungua kongamano la wadau wa elimu ya watu wazima, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima na elimu nje ya mfumo rasmi, kongamano hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. (PICHA NA FRANCIS DANDE).
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Wazima. Dk. Michael Ng'umbi, akizungumza wakati wa kongamano la wadau wa elimu ya watu wazima, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu
Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akipokea zawadi alipotembela banda la TEA.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge, akiangalia kitabu chenye matokeo ya kidato cha Nne ya Mwaka 1975. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Maktaba ya Taifa, Dk. Mboni Ruzegea.
Mgeni rasmi akipita kata baadhi ya mabanda ya washiriki wa kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeweka mikakati ya kukabiliana na changamoto ya kushuka kwa kiwango cha wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) katika kipindi cha mwaka 2022/2023 na 2024/205.
Mkakati huo unalenga kukuza na kuendeleza Kisomo cha Elimu ya Umma (MTaKEU).
Akizungumza leo Oktoba 19, 2022 katika Kongamano la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salam (DUCE), Kamishna wa Elimu nchini Dkt Lyabwene Mtahabwa amesema mkakati huo umeandaliwa kwa makusudi kama nyenzo ya kuongoza wadau mbali mbali ambao wanatekeleza program za kimasomo.
Amesema mpango huo unatambua kisomo kama haki ya msingi kwa maendeleo ya mtu binafsi, kijamii, kiuchumi na kisiasa.
“Vile vile, Wizaa imeandaa miongozo mitano ambayo inasaidia katika utekelezaji wa kuimarsha ubora wa utolewaji wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP).” Amesema.
Amesema mpango huo umelenga kuwapa fursa ya kuendele ana masomo vijana walio nje ya mfumo rasmi hususani wasichana waliopata ujauzito.
Dk. Mtahabwa amesema katika kipindi cha mwaka 2021 jumla ya wasichana 3,333 walijiunga na program hiyo katika vituo 131 nchi nzima.
“Haya ni baadhi ya mambo yaliyofanywa na serikali, hivyo nawaasa wadau wote kutumia kongamano hili kujadili na kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya ujifunzaji katika progrmu za kimasomo yanayozingatia ubora, usawa na ujumuishi kwa makundi yote.” Amesema.
Amesema kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na UNESCO hivi karibuni, kiwnago cha watu wazima wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu ni asilimia 77.89 hali ambayo imeelezwa si mbaya ingawa nchi imerudi nyuma ukilinganisha na miaka ya nyuma.
“Kupitia kongamano hili, watendaji mlitumie kuweka mikakati thabiti ya kuondoa changamoto ya kutojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu nchini, ni dhahiri Taifa lenye watu walioelimika ni rahisi kuleta maendeleo yatakayoweza kubadili maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.”Amesema.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge akifungua Kongamano hilo amesema lengo la maadhimisho hayo ya juma la Elimu ya Watu Wazima ni kujenga uelewa na kutambua changamoto mbali mbali zinazoikabili tasnia hiyo kwa jamii na dunia kwa ujumla.
“Ni imani yangu tutaweza kubadilisha mitizamo juu ya mipango, uendeshaji, usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi ili kuendana na dira ya maendeleo yam waka 2025.” Amesema.
Amesema pia malengo ya maendeleo endelevu ya 2030 hasa katika lengo namba nne ambalo linalenga kuhakikisha vijana na watu wazima wote wanaume na wanawake wanafikia kiwango cha kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesababu ifikapo 2030.
No comments:
Post a Comment