Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akishiriki kumhudumia mteja wakati alipotembelea kituo cha kutolea huduma kwa wateja cha Airtel ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma ya wateja.
Dar es Salaam Alhamisi 6 Oktoba 2022, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Haabri Nape Nnaye leo ameshiriki kwenye maonyesho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaondaliwa na kampuni ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo ambayo yalianza tangu mwishoni mwa wiki ni kwa ajili ya kuleta wateja wa Airtel kwa ukaribu, kujua changamoto zao na kuweza kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma za mawasiliano yaliyo bora.
Akizungumza baada ya kumalizika kutembelea maonyesho hayo, Waziri Nnauye alitoa pongezi kwa Airtel kwa kuweza kuendelea kuboresha huduma zake. ‘Naomba nichukue fursa kuwafahamisha Watanzania kuwa Airtel ni kampuni inayomilikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 49 kwa hivyo ni muhimu kutambua kuwa wanapotumia huduma za Airtel wanatumia kilicho chao’, alisema Nnauye.
‘Nimefurahi kuona jinsi Airtel imejipanga kuwahudumia Watanzania huku ikiendelea kuboresha huduma zake. ‘Serikali imekuwa ikiwahimiza watoa huduma kuangalia namna ya kusaidiaWatanzania kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kuongeza upatikanaji wa simu njanja. Kwa kuona na kutambua umuhimu huo, Airtel imekuja na njia ya kutoa simu njanja kwa mkopo, ambapo mteja analipia elfu 70 na kisha kumalizia kwa kulipa kidogo kidogo’, alisema Nnauye.
‘Natoa shukrani kwa niaba ya serikali kwa watoa huduma za mawasiliano akiwemo Airtel kwa kazi nzuri mnayo endelea kufanya na mpaka kutambulika na Shirikisho la Mawasiliano Duniani na hatimaye kuweza kuchanguliwa kuingia kwenye Baraza hilo kwa kupata kiti katika ya 48. Hii ni kazi nzuri ambayo watoa huduma za mawasiliano wamekeza na nawapongeza sana.
Waziri Nnauye pia alitembelea kituo cha kutoa huduma kwa wateja na kushiriki kwenye kusikiliza na kutatua baadhi ya changamoto kutoka kwa Wateja wa Airtel.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Dinesh Balsingh alimpongeza Waziri Nnauye kwa kushiriki wiki ya huduma kwa wateja, na kusema imeleta hamasa kubwa kwa wafanya kazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma za hali ya kimataifa.
‘Wiki ya Huduma kwa wateja inatoa fursa nyingine kwa Airtel kujiweka karibu na wateja wake ambao ni watu muhimu sana kwenye biashara yetu. ‘Huku kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja ikiwa ni furahia huduma, Airtel inajivunia kwa Watanzania kuwa wateja wetu na tunahidi kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa, alisema Balsingh.
‘Moja kati ya hatua ambazo Airtel tuweza kuzipiga vizuri na tunazojivunia ni teknolojia. Tunayo furaha kubwa kuwa kwa sasa wateja wetu wanaweza kutumia teknolojia na kujihudumia papo hapo. Wateja wa Airtel kwa wanaweza kupata LUKU TOKEN kwa kujihudumia mwenyewe, kurudisha muamala uliokosewa, kurudisha laini ya simu iliyopotea bila kuongea na mtoa huduma wa Airtel. Huduma zote hizi mteja anaweza kuzipata kwa urahisi na hii ni moja ya faraja yetu tunayojivunia kwenye teknolojia kama watoa huduma, aliongeza Balsingh.
No comments:
Post a Comment