Na Mwandishi Wetu
Halijawaka wala Haijanyesha lakini ngoma sare sare mauwa, mechi dume ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)
Dakika 90 za kwanza zimetamatika kwa Yanga kulazimishwa sare ya bao (1-1) matokeo ambayo sio mazuri licha ya kuwa na dakika 90 za kujiuliza mjini Khatoum nchini Sudan wiki ijayo.
Si matokeo mazuri kwa Yanga kwa sababu walihitaji tofauti kubwa ya mabao katika uwanja wao wa nyumbani, kwa matokeo haya maana yake ni lazima akafunge bao ugenini, sare ya 0-0 amepita Al Hilal, hapa pia inatategemea wao wanakwenda vipi kuzuia kule Omdurman, mechi imekuwa ngumu zaidi kwao kuliko Al Hilal kutokana na nature ya mashindano ya CAF, mtu anashinda kwake.
Florent Ibenge alikuja na game approach ambayo ilifanikiwa katika matendo ya mwendo, Al Hilal ilikuja na mpango kazi wa kucheza dhidi ya namna ya uanzishwaji wa mashambulizi ya Yanga, waliwatia presha Yanga wakiwa na mpira wachezaji watano wanakuwepo katika nusu ya Yanga ili waanze kukabia juu.
Kuna nyakati ambazo Yanga walifanikiwa lakini katika nyakati ambazo Yanga ilifika kwenye eneo la mwisho bado ilimkosa mtu ambae anaweza kuutuliza mchezo, timu ikakosa utulivu.
Mapema kipindi Cha pili bao la Fiston Mayele likawamusha Al Hilal waliamua kukabia katikati mwa uwanja Ili kuziba mianya ambayo Yanga walichotaka kuzitumia na kushambulia kwa mashambulizi ya kushitukiza bao likapatikana.
Mkoba wa mbinu za Mohammedi Nabi ni kama alijifunga, mosi kukosa kiungo wa kunusa hatari na mwenye sifa za ukabaji Ili aweze kuziba mianya kati ya viungo washambuliaji na mabeki wa pembeni.
Al Hilal waliendelea kutumia udhaifu huo bahati nzuri kwa Yanga ni ubora na bahati kwa ya mlinda mlango wao Digui Diarra akiokoa zaidi ya nafasi tatu za wazi.
Ni kibarua kizito kwa Yanga mosi kukubali presha ya wasudan lakini pia kukabiliana na Ufundi wa vijana wa Florent Ibenge.
No comments:
Post a Comment