HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 18, 2022

  Dawa za kulevya zamuibua Askofu Mwamalanga

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga  ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kuwataja wahadharani watu wanaodaiwa kujishughulisha na biashara hiyo haramu.

Askofu Mwamalanga ametoa pongezi hizo siku chache baada ya Kamishina  Mkuu wa DCEA, Gerlad Kusaya kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuwataja hadharani   watuhumiwa wa dawa za kulevya tisa ambapo wanadaiwa kukutwa na kilo 34.89 ya heroine  jijijini Dar es Salaam  hivi karibuni.

Waliokamatwa ni mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Dar es Salaam, Kambi Zuberi Seif, Muharami Sultan (40) na John John, maarufu Chipanda (40) ambaye jukumu lake ni kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kwenye kituo hicho. 

 

Wengine ni Said Matwiko, mkazi wa Magole, Maulid Mzungu maarufu Mbonde (54) mkazi wa Kisemvule, Rajabu Dhahabu (32) mkazi wa Tabata, Seleman Matola Said (24), mkazi wa Temeke Wailes, Hussein Pazi (24) mfanyabiashara na Ramadhani Chalamila (27) mkazi wa Kongowe.

“Sisi viongozi wa dini  tunaona huu ni ushindi  mkubwa  kuwahi kutokea  hongera  sana  mamlaka ya kupambana na  dawa za  kulevya nchini  kwani kwa muda mrefu  sasa Watanzania  wamekuwa wakipiga kelele juu ya kuibuka upya biashara  hiyo haramu,” alisema

Mwamalanga alisema kuibuka kwa biashara hiyo kumekuwa kukihusihwa na vyombo vya michezo na baadhi  ya madhehebu ya dini, hivyo kuishauri mamlaka hiyo kuongeza nguvu katika mapambano.

Alisema miaka ya nyuma  viongozi wa  dini  wakiwamo Mashekhe  na Maaskofu  walitoa orodha  ndefu ya waingizaji wakubwa wa dawa za kulevya  nchini,  lakini hakikufanyika chochote.

“Ndiyo maana tuipongeza mamlaka hii kwa kuthubutu.   Hakika  tukuombea dua  ya ulinzi Kamishna Kusaya kwa Mwenyezi Mungu aendelee kukupa ulizni wa kufanya kazi yako kwa weledi, katika  kulilinda Taifa dhidi ya dawa za kulevya....

Tunahimiza viongozi wakuu wa michezo nchini  kujisafisha na kusafisha timu zao ili zisitumike  na wahalifu  wachache   kuliangamiza  Taifa  kwa tamaa zao za utajiri  wa haraka bila baraka,” alisema.

Aidha, Askofu Mwamalanga alisema wanamuomba Kamishna Kusaya kuisafisha mamlaka hiyo kwa kuwaondoa baadhi ya  watendaji  ambao wanatajwa kuficha wahalifu  pindi wanapowakamata kwa kupewa rushwa  kubwa   za magari na pesa. 

“Ni vema chombo  kikafanya kazi zake kwa uwazi,  bila kulinda  wahalifu  wanaotumia  dini na michezo  kusafirisha  dawa za kulevya...sisi tumejipa jukumu la kukemea   na kutoa  ushirikiano  wa kila siku kwa mamlaka, ili Tanzania  bila dawa za kulevya  isomeke kwa vitendo,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Pages