Na Mwandishi Wetu
NI 'TOTAL DOMINANCE ' kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90 ya Mchezo Yanga SC dhdi ya Singida Big Stars.
Unaweza sema Kati ya dakika 45 bora ambazo Yanga wamecheza msimu huu katika ligi mpaka sasa. Walicheza na swagga ( ufundi , sanaa, maarifa na Nguvu )
Kwenye mfumo wao wa 4-2-3-1 , Aucho Bangala na Feisal katikati ya uwanja ndio waliamua mechi , siku zote kwenye mpira kitu muhimu ni nafasi na viungo watatu wa Yanga walikuwa wanaipata nafasi haraka na kwa nyakati sahihi matokeo yake viungo wa SBS walikuwa wanafukuza vivuli uwanjani.
Singida Big Stars ni kama hawakuwa tayari katika hii mechi , walikuwa wapo taratibu, pasi hazifiki, wanachelewa kufika kwenye matukio mengi ya mpira wa kwanza na hata kwenye mipira ya pili, hasa kwenye kiungo na pembeni ya uwanja . 4-4-2 yao ilikuwa wazi sana hasa kwenye mistari yote mitatu ulinzi kiungo na ushambuliaji.
Singida Big Stars wakiwa na mpira wanakuwa mbali sana kupigiana pasi na wakipoteza wanakuwa mbali sana kufunga nafasi , na hapo ndio Yanga walipokuwa wanatoa adhabu ..... adhabu ya mabao na adhabu ya kuwanyima mpira kwa muda mrefu.
Kipindi cha pili baada ya Hans kufanya mabadiliko ya umb kutoka 4-4-2 na kwenda 4-2-3-1 , Kaseke akiingia katikati ya uwanja akiunganika na Ndemla na Bruno wakiwa na mpira wanakuwa 4-2-3-1 wakiupoteza wanakuwa 4-3-3 , nia kubwa ni kupunguza utawala wa Yanga katikati ya kiwanja , na kwa kiasi kikubwa ilifanya Singida kipindi cha pili kuwa imara.
Hat Trick kwa King Mayele, umaliziaji wa kiwango cha juu kwa magoli yote matatu. Hadi dakika 90 Yanga (4-1) Singida Big Stars.



No comments:
Post a Comment