HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 04, 2022

HAWA MWAIFUNGA ATOA USHAHIDI KESI YA AKINA MDEE

 

Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga (kushoto), akiteta jambo na wakili wake Edson Kilatu, baada ya kutoa ushahidi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi iliyofunguliwa na wabunge wa Chadema waliovuliwa uanachama. (PICHA NA FRANCIS DANDE).


Na Mwandishi Wetu

 

MBUNGE wa Viti maalum kupitia Chadema, Hawa Mwaifunga amedai mahakamani kwamba nafasi pekee waliyopewa na Baraza Kuu la Chama hicho ni kuomba msamaha.


Mwaifunga alidai hayo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati akijibu maswali ya wakili wa Chadema Peter Kibatala dhidi ya kesi iliyofunguliwa na kina Halima Mdee kupinga kuvuliwa uawanachama wa chama hicho.

Alidai mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, kuwa yeye na wenzake 18 waliitwa kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la Chadema Mei 11 mwaka 2022 ambapo katika kikao hicho walitakiwa kuthibitisha rufaa zao.

Mbunge huyo alidai nafasi nyingine waliyopewa ni kuomba msamaha kabla wajumbe wa baraza hilo kupiga kura na hafikia uamuzi wa kutangaza kuwavua uanachama wao.

"Uamuzi wa baraza hilo ulitokana na utaratibu  wa kupiga kura kila kanda, wajumbe 23 wa Kamati Kuu ya Chadema wakipiga kura hizo peke yao.

"Idadi ya kura zilizopigwa na wajumbe hao ni 423 ambapo 413 walikubaliana na uamuzi wa kutuvua uanachama, watano walikataa uamuzi na watano hawakuwa na upande,"alidai.

"Katika kiapo changu sikueleza kama Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu John Mnyika walikuwepo katika kikao cha Baraza Kuu kilichowafukuza uanachama kwasababu Katiba ya chama hicho inaeleza wanaoongoza vikao vya kufanya maamuzi, "alidai mbunge huyo.

Mdee na wenzake 18 wanapinga kuvuliwa ubunge na Baraza Kuu la Chadema.

No comments:

Post a Comment

Pages