Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma leo.
Serikali imejenga Kituo cha Askari Wanyamapori Wilayani Itilima mkoani Simiyu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu pembezoni mwa Pori la Akiba la Maswa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Daudi aliyetaka kujua lini Serikali itajenga Kituo cha Askari Wanyamapori Wilayani Itilima na maeneo yanayozunguka Pori la Akiba Maswa.
Amesema kituo hicho kitakachohudumia zaidi ya vijiji tisa kitakuwa na askari wa jeshi la Uhifadhi na Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika vijiji vya Longalombogo, Nding’ho, Lung’wa, Nyantugutu, Mbogo, Shishani, Pijulu, Ng’walali na Mwamakili.
Mhe. Mary Masanja ameongeza kuwa Pori la Akiba la Maswa lina vituo vidogo sita vya askari vinavyotumika kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na kwamba Wizara hiyo imeandaa Mpango wa kuwatumia Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) wa wilaya husika watakaopewa mafunzo ili kusaidiana na Askari wa Jeshi la Uhifadhi katika kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu.
“Awamu ya kwanza ya mafunzo imefanyika mwezi Oktoba na imehusisha Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) 37 kutoka Wilaya 9 ikiwemo Wilaya ya Itilima iliyotoa Askari wanne, Wilaya ya Busega, Meatu, Bunda, Tunduru, Nachingwea, Lindi Vijijini,Rufiji na Liwale”





No comments:
Post a Comment