Na John Richard Marwa
VIWANGO, Viwango, Viwango tu kwenye Ligi ya Mabingwa Soka la Wanawake Afrika (CAF WCL) katika makala ya pili ya Mashindano hayo tangu kuanzishwa kwake msimu uliopita.
Kikosi cha Simba Queens kimeandika rekodi mpya Barani Afrika kwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo baà da ya kuwatwanga Green Buffalos ya Zambia kwa mabao (2-0) .
Ulikuwa mchezo wa kufa ama kupona kwa Simba Queens ambao walikuwa wanahitaji kushinda tu ili kusonga mbele wakati wapinzani wao wakihitaji sare yoyote Ile ama kushida kuweza kufuzu hatua ya Nusu Fainali.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote mbili licha ya Simba kuwa na takwinu bora katika maeneo yote ya Uwanja.
Mwalimu Charles Lukula alikuja na mabadiiko ya safu ya kiungo na ushambuliaji, kwa kumuacha nje Asha Djafar na kuanza na Philomena Abaka, Vivian Corazone nafasi yake akicheza Fetty Densa ambaye alitengeneza uwiano mzuri na Joelle Bukulu.
Kipindi cha pili Simba Queens waliingia kwa kushinikiza mashambulizi huku nidhamu ya ulinzi ikiwa juu kwa maana Green Buffalos walikuwa wanacheza kwa mashambulizi ya kushitukiza.
Alikuwa ni Asha Djafar alitetokea benchi dakika ya 38 ya mchezo kuja kuandika bao kipindi cha pili akiunganisha kross safi ya Fetty Densa.
Bao hilo liliwavuruga vijana wa Green Buffalos nabkuanza kuhanikiza mashambulizi na Simba wakatumia mianya waliyokuwa waniacha kumaliza mchezo.
Oppah Clement alipigilia msumari wa mwisho kwa kuiandikia Simba bao la pili la ushindi.
Kwa ushindi huo Simba Queens wameadika historia kuwa klabu ya kwanza kutoka ukanda wa cecafa kushiriki kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo.
Simba Queens wamefikisha point sita nyuma ya vinara As Far waliomaliza katika nafasi ya kwanza wakishinda mechi zote tatu za hatua ya makundi.





No comments:
Post a Comment