HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 16, 2022

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA SERA YA UBIA YA NHC

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa  sera ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwa katika uzinduzi wa sera ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa  sera ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.



Na John Richard Marwa

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha linajenga miji na majiji katika mandhari ya kupendeza kwa ajili ya makazi ya watu.

Ameyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Shirika la Nyumba la Taifa mna uwezo wa mkubwa sana kubadilisha miji na majiji yetu na mandhari yake maana nyie ndio mnamiliki majengo mengi yaliyo katikati ya majiji yetu"

"Kama ambavyo Mkurugenzi ameeleza kwamba Shirika hili lazima liwe mfano katika ujenzi wa nyumba bora kwenye mikoa yote nchini na hili ndilo Shirika ambalo lmepewa jukumu la ujenzi wa nyumba bora kwenye maeneo yetu" Waziri Majaliwa ameongeza kuwa.

"Jengeni miji iwe ya kisasa zaidi, mandhari nzuri ya kupendeza zinahitajika zaidi na sisi tufanane na maeneo mengine, wivu wa kuiga mambo mazuri ni mzuri zaidi kuliko wivu wa kuchukia hivyo basi Shirika la Nyumba la Taifa muwe na wivu wa kuiga wenzetu kujenga miji yetu"

"Nina Imani kuwa kazi mliyonayo ya kujenga Nyumba za watu hasa wenye kipato cha kati itawasaidia sana kupata fedha za kuweza kuwafikia Watanzania wenye kipato cha chini ili na wao waweze kunufaika"

"Serikali kwa upande wetu tutaendelea kuboresha sera na sheria mbalimbali ili kusaidia vyombo vya fedha kupunguza riba za mikopo ili kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa sekta ya nyumba kuweza kukua na kuwawezesha Watanzania" ameongeza kuwa

"Ni Imani yangu kuwa baada ya uzinduzi wa Sera hii Shirika litafanya uchambuzi na kutoa matokeo kwa waleta maombi yawe ya ujenzi wa nyumba hapa ni kupata wawekezaji ambao hawataishia njiani ili kukamilisha miradi yao husika."

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais anaamini kuwa sekta ya nyumba itaendelea kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika utekelezaji wa jambo hilo lenye manufaa kwa maendeleo ya makazi na uchumi wa Taifa.

Kwa upande wa Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula akimkaribisha Waziri Mkuu kuzindua sera hiyo ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa amesema Ili kutekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria ni lazima kuongea ushiriki wa sekta binafsi.

"Ili kutekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria ya kutimiza adhma ya Serikali inayoongozwa na Mhe, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa mambo ya Serikali.

"Shirika la Nyumba limefanya maboresho makubwa ya Sera yake ya Ubia na sasa iko tayari kwa ajili ya kuzinduliwa ambayo tumekualika uweze kuzindua.

"Maboresho hayo yalikuwa yamelenga zaidi utekelezaji wa miradi ya Ubia lakini pia kuongea tija zaidi kwenye Shirika na wawekezaji kwa ujumla.

Nae Mkurugenzi wa NHC Nehemia Mchechu amesema "Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekuwa likitekekeza miradi ya ujenzi na umiliki wa majengo kwa njia ya ubia na wawekezaji binafsi au sekta ya umma. Miradi hiyo iliekelezwa kwa kufuata Sera ya Ubia ya Shirika ya 1993 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1998, 2006 na 2012. Aidha marekebisho mengine yamefanyika mwaka 2022 yakilenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ubia.

"Ardhi ya Shirika haitatumika kama dhamana ya mkopo utakaotumika katika uendelezaji wa mradi wa ubia. Shirika litaingia mikataba ya ubia na makampuni au taasisi zilizosajiliwa tu." amesema Mchechu.

No comments:

Post a Comment

Pages