HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 02, 2022

YANGA HOI KWA CLUB AFRICAIN

 


 Na Mwandishi Wetu


Klabu ya Young Africans wameshindwa kutamba wakiwa nyumbani leo dhidi ya Club Africain ya Tunisia mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC.


Yanga waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri Ili kujiwekea mazingira mazuri katika mchezo wa mkondo wa pili nchini Tunisia.


Haikuwa mechi rahisi kwa Yanga kutokana na jinsi ambavyo Club Africain walikuwa wanacheza kwa kutotoa nafasi kwa washambuliaji wa Yanga.


Mwalimu Nabi alianza na mfumo wa 4:2:3:1 kianza na Aucho na Feisa kwenye kiungo cha ulinzi huku Aziz Ki, Morrison na Kisinda kwenye safu ya viungo wa ushambuliaji na Mayele akisimama pekeake.


Mpango wa Yanga ulikwama kwenye namna ya kuifungua safu ya ulinzi ya Club Africain kwani walikuja na mfumo wa 4:5:1 wakiziba mianya yote kwa viungo wa ushambuliaji wa Yanga kushindwa kuwa na mikimbio chanya ama kujitengenezea nafasi.


Mosi Club Africain waliwalazimisha Aziz Ki, Feisal na Aucho kucheza kwenye mstari mmoja jambo ambalo iliwalazimu Yanga kuanzisha mashambulizi kupitia kwenye mapana ya uwanja huku wakikosa ubora wa Morrison na Kisinda kuushambulia mstari wa ulinzi.


Kipindi cha pili mchezo uliendelea kwenye biti ileile na Club Africain wakazidi kuwa bora kwa mpango wao wa kujilinda uliufanya mchezo kuwa mlima mrefu kwa Yanga kwa kukosa mbinu mbadala za kuucukua mchezo.


Club Africain walikuwa bora sana kwa mpango wao wa mchezo waliokuja kucheza wakiwa wanahitaji kupata sare wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa marejeano.


Ikumbukwe kuwa Club Africain hatua iliyopita waliwatoa Kipanga FC ya Zanzibar kwa kuwafunga mabao 7-0 huku mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar wakipata Suluhu kama walivyofanya leo kwa Yanga.


Dakika 90 za kwanza zimetamatika kwa Yanga kutoka suluhu na Club Africain huku ukisumbuliwa mtanange wa mkondo wa pili utakaochezwa November 9 nchini Tunisia.

No comments:

Post a Comment

Pages