HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 24, 2022

 DERBY YA SIMBA QUEENS, YANGA PRINCESS MBUNGI YAMWAGIKA

Na John Richard Marwa

Ilipigwa mbungi, ikapigika, Watu wakafurahi. Zilikuwa dakika 90 za haja kwa pande zote. Simba Queens wakiwaalika Yanga Princess Benjamin Mkapa mchezo wa Ligi Kuu Soka la Wanawake Tanzania Bara (SWPL) ulitamatika kwa sare ya bao (1-1).

Baada ya mchezo huo kumalizika umeibua mijadala mingi kwenye vijiwe vya kidigitali kutokana na ubora wa mchezo wenyewe na ubora wa mchezaji mmoja mmoja ulioonekana.

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema nae ameibuka na kutia neno kupitia ukurasa wake wa Instagram juu ya mchezo huo ambao umzidi kujitwalia mashabiki lukuki.

Lema amesema mchezo wa Soka la Wanawake linazidi kupiga hatua kila uchao kutokana na mafanikio ambayo yamekuwa yakipatikana kwa ngazi ya Kimataifa.

"Sitaki kuyazungumzia sana matokeo ya jana, nataka kuizungumzia ladha ya soka la wanawake inavyokuwa kwa kasi tumestrugle muda mrefu sana kwenye mpira wa wanawake, kwa sasa kadri siku zinavyozid kwenda ubora unaongezeka, ni ngumu kusema tunaweza kufikia level ya wanaume lkn ukweli ni kwamba tumepiga hatua kubwa.

"Timu za Taifa zimekuwa zikifanya vizuri na kufanikiwa pia kucheza kombe la Dunia, na ni juzi tu Tanzania imewakilishwa kwenye mashindano ya Club bingwa ambao ni Simba Queens na kufika hatua ya nusu fainal,
Kuna wachezaji wametokea kwenye ligi hii wameenda kucheza ulaya tena vilabu vikubwa na wengine ambao sio watanzania hii ni hatua kubwa pia." Ameongeza kuwa.

"Leo tunaweza kushuhudia derby yenye wachezaji kutoka mataifa yasiyopungua sita kwenye mechi moja sio jambo dogo huko tunakoamini kwamba wako juu kuliko sisi lkn wao wameona Tanzania kuna ligi bora kuliko kwao hili jambo la kujipongeza pia, tuanze kuipongeza TFF na Vilabu ambavyo vimeamua kuwekeza kwenye soka la wanawake.

"Pia kuifanya ligi yetu ya wanawake kuwa bora, Tunatamani kuwaona watoto wetu wakifaidika na vipaji vyao kupitia soka hili la wanawake, naamin baada ya muda mchache thamani yao itapanda maradufu."

Hata hivyo Kocha huyo mwenye tambo nyingi alimalizia kwa kusema kuwa .

"NB: Ile mechi ya jana ilipaswa kuendelea kuchezwa mpaka sasa, mechi bora iliyoikaribisha skukuu, hahahaha!".


No comments:

Post a Comment

Pages