Maandalizi ya mwisho kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu yakiendelea.
NA TULLO CHAMBO
TAMASHA la 21 la Michezo la Karatu 'Karatu Sports Festival 2022' linatarajiwa kufikia tamati kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu, kesho Jumamosi Desémba 24.
Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo, Meta Petro, tamasha hilo linalofikisha mwaka wa 21 sasa tangu kuanzishwa kwake, lilianza takribani wiki moja kwa michezo mbalimbali na litafikia tamati kesho kwa mchezo wa riadha na baiskeli, sambamba na ngoma za asili na kwaya.
Meta, alisema leo Ijumaa mpira wa Wavu fainali yao inafanyika mjini Karatu wakati Soka ni Uwanja wa Basodawishi.
Alisema, kesho Jumamosi shughuli pevu itakuwa kwenye Uwanja wa Mazingira Bora, ambapo wanariadha mbalimbali nchini wakiwamo magwiji, wataoneshana kazi.
Pia, alisema Baiskeli watakuwa na shughuli pevu kwenye barabara mbalimbali za mjini Karatu.
Fainali hizo, pia zitapambwa na ngoma za asili, kwaya na sarakasi.
Tamasha hilo, huandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), chini ya udhamini wa Olympic Solidarity (OS), Shule za Filbert Bayi na kuratibiwa na Meta Promotions.
No comments:
Post a Comment