HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2022

IDDI PIALALI,NDOGA WAONGOZA MABONDIA KUPIMA AFYA USIKU WA MABINGWA

Mabondia Iddi Pialali aongoza mabondia kupima afya kuelekea Pambano La Usiku Wa Mabingwa Litakalopigwa Desemba 26, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa AICC Arusha.


Akizungumza wakati wa upimaji afya jijini Dar es Salaam Iddi Pialali amesema wanamasumbwi watarajie kushuhudia mfaume Mfaume akimtwanga TKO kwenye Pambano hilo.

Kwa upande wake bondia namba moja kwa Wanawake Tanzania Halima Vunja Bei amesema yeye ni mkongwe hivyo mpinzani atarajie kipigo cha aina yake.

Mratibu Msaidizi kutoka Peaktime, Bakari Hatibu, amesema hii ni ishara njema ya watanzania kushuhudia burudani ya aina yake katika pambano la kufunga mwaka la Usiku wa Mabingwa kati ya Iddi Pialali na Mfaume Mfaume.


Mvutano mkali wa tambo za mashabiki ukiendelea katika mitaa ya Mabibo na Mazense kuelekea pambano la Kufunga Mwaka La Usiku wa Mabingwa litakalo kutanisha miamba miwili Mfaume Mfaume mapafu ya mbwa dhidi ya iddi Pialali huku Karim Mandoga akimkabili Alibaba Ramadhan kutoka Moshi kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa AICC Arusha.


No comments:

Post a Comment

Pages