HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2022

 WANARIADHA WAPENYA PROGRAMU YA OLIMPIKI PARIS 2024


Katibu Mkuu WA TOC, Filbert Bayi (wa pili kushoto mbele), akiwa katika picha ya pamoja washindi wa mita 200 wanawake. Nyuma yake ni Winfrida Makenji, aliyefanikiwa kufikia viwango vilivyokuwa vimewekwa.

 Makamu wa Rais wa TOC, Henry Ben Tandau, akiwasoma washindi mbalimbali katika mashindano maalumu ya kusaka viwango kuelekea Olimpiki Paris 2024, yaliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 Wanariadha mbalimbali waliojitokeza kushiriki mashindano hayo.

 

NA TULLO CHAMBO

WANARIADHA wanne wamefanikiwa kufikia viwango vya kuingia katika mpango maalumu wa Tanzania, kuelekea michezo ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa 2024.


Wanariadha hao, wamefanikiwa kufikia muda, katika mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), yaliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar   es Salaam, leo Jumapili Desemba 18 na kushirikisha wanariadha mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani.


Kwa kufanikiwa kufikia viwango hivyo, mbali na kujishindia medali na fedha taslimu, wataingia katika programu maalumu ya TOC ikiwamo kuanza kuandaliwa hivi sasa kwa kambi kuelekea Paris 2024.


Wanariadha hao ni pamoja na Ali Khamis Gulam kutoka Zanzibar, aliyeshinda mbio za Mira 100 wanaume akitumia sekunde 10:40 huku muda uliokuwa umewekwa na TOC ni 10:4.
Mwingine ni Winfrida Makenji pia kutoka Zanzibar, aliyekimbia mita 200 wanawake, akitumia sekunde 23:80 huku muda uliokuwa umewekwa ni 23:09.


Gulam, alifanikiwa tena kufuzu katika mita 200 akishika nafasi ya kwanza akitumia sekunde 21:07 huku muda uliokuwa umewekwa ni 21:08 huku pia mshindi wa pili Benedicto Mathias akipenya kwa sekunde 21:74.


Mashindano hayo yalishirikisha mbio za Mira 100, 200, 400, 800, 1500, 5000 na mitupo.

No comments:

Post a Comment

Pages