Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Baraza
la Ushauri wa Huduma za Usafiri wa Ardhini (LATRA) limetoa mapendekezo
ya Nauli za Treni ya Mwendokasi (SGR) kwa Daraja la kawaida kutoka Dar
es Salaam Hadi Morogoro kwa Sh 24,794 kwa Mtu Mzima wakati kwa mtoto
mwenye umri wa miaka 4-12 anatarajiwa kulipa Sh 12,397.
Akizungumza
katika Mkutano uliowakutanisha Wadau wa Usafiri nchini jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA),
Habibu Juma Saidi Suluo amesema kuwa kwa Daraja la Kati kutoka Dar es
Salaam kwenda Morogoro gharama ya Nauli inatarajiwa kuwa Sh 29,752
wakati kwa mtoto mwenye umri wa miaka Kati miaka hiyo hiyo itakuwa ni Sh
14,876.
"Kwa
upande wa Nauli ya kutoka jiji la Dar es Salaam hadi Dodoma kwa Daraja
la kawaida mtu Mzima anatarajiwa kulipa Sh 59,494 wakati mtoto
anatarajiwa kulipa shilingi 29,747". Amesema Suluo.
Suluo
ameongeza kuwa nauli kwa Daraja la Kati kwa mtu mzima anatarajiwa
kulipa Sh 71,392 huku mtoto natarajiwa kulipa Sh 35,696.
Awali
Mkuu wa Wilaya ya IIala, N'gwilabuzu Ludigija akimwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Malala amesema Serikali ya awamu ya sita
imelenga kuboresha Miundombinu ili kuweza kumrahisishia mwananchi.
"Katika
kuhakikisha tunaboresha huduma za reli kesho tunatarajia kusaini
mkataba wa Ujenzi wa Reli kutoka Kigoma hadi Tabora". Amesema Ludigija.
Ameongeza
kuwa kutokana na usafiri huo kuwa ni muhimu nchini ameishauri taasisi
hiyo isiridhie nauli hizo mpaka watakapofikia makubaliano ya wadau wa
usafiri nchini juu ya nauli hizo.
"Kila mmoja aliyeopo hapa ajisikie na awe huru kutoa maoni yake kwa lengo la kupata mapendekezo bora". Amesema Ludigija.
No comments:
Post a Comment