HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 17, 2022

MWAMPOSA APEPERUSHA MASHINDANO YA OLIMPIKI BENJAMIN MKAPA

 

Wachezaji wakipewa taarifa na viongozi wao, kutokana na sintofahamu iliyosababisha mashindano kushindwa kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


 Jukwaa lililosababisha mashindano ya Riadha kushindwa kufanyika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

 

 Na Mwandishi Wetu

 

MASHINDANO ya Riadha ya siku mbili kusaka viwango vya kushiriki Michezo ya Olimpiki Paris 2024, yameshindwa kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar  es Salaam.

 
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kushirikisha wanariadha kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar, yalikuwa yafanyike kuanzia leo Desemba 17 na 18.

Mashindano hayo, yameshindwa kuanza leo, kutokana na athari zilizosababishwa na mkesha wa Tamasha la Dini la Apostle Boniphace Mwamposa 'Bulldozer', usiku wa kuamkia leo, uwanjani hapo.

Mwamposa, alifunga jukwaa kubwa kwenye sehemu ya kukimbia (running track', hivyo kufanya uwanja huo kushindwa kutumika, kwani hadi saa tisa mchana, lilikuwa halijafunguliwa na kulikuwa hakuna dalili za kufunguliwa.

Licha ya juhudi za Msimamizi Mkuu wa Mashindano hayo, Sunday Burton Kayuni na Meneja wa Uwanja huo, Daniel Madenyeka, kufanya juhudi za kuwasiliana na wahusika kulifungua, juhudi ziligonga mwamba.

Kutokana na tatizo hilo, sasa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika leo uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

Pages