NA STEPHANO MANGO, NAMTUMBO
MASHINDANO ya Mbunge na Mantra Wilayani Namtumbo yaliyoshirikisha timu 14 kutoka kata zote yamekamilika kwa timu ya Rwinga kuibuka mshindi dhidi ya timu ya Lusenti ambao wameibuka mshindi wa pili katika ligi hiyo ya mtoano.
Mratibu wa mashindano hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Namtumbo (Nadifa) Zuberi Kossa alisema kuwa Mshindi wa mashindano hayo ni timu ya Rwinga ambayo imejichukulia zawadi ya kombe, fedha taslimu laki sita, na mpira mmoja, pia mshindi wa pili ambaye ni Lusenti imejichukulia zawadi ya shilingi laki nne na mpira mmoja.
Kossa alisema pia mshindi wa tatu amejinyakulia zawadi ya shilingi laki mbili na mpira mmoja na kwamba zawadi nyingine ambazo zimetolewa na mdhamini wa mashindano hayo ni kwa mchezaji bora, kipa bora , kocha bora na timu yenye nidhamu kwa kila kipengele imetolewa shilingi elfu kumi.
Mratibu huyo alisema kuwa mashindano hayo yalishirikisha
timu kutoka kata 14 za Kitanda, Mchomoro,Luegu,Luchili,Mputa,
Kossa alisema kuwa tunamuomba mdhamini na wadau wengine wa michezo waweze kuboresha mashindano hayo ili yaweze kuleta furaha na tija kwa wadau wote kuwa ni Pamoja na mashindano hayo yaanze mwezi juni na kumalizika mwezi septemba.
Pia alisema mashindano hayo yaanzie katika ngazi ya vilabu katika vijiji na kupanda katika ngazi zingine, kuleta wataalamu wa michezo ili kuwafundisha wataalamu watakaosaidia kuinua viwango vya michezo, Pamoja na kuwasaidia seti za jezi waamuzi.
Akizungumza uwanjani hapo Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa alisema kuwa mashindano hayo yalianzishwa kwa lengo la kuwanufaisha wananchi na wakazi wa Namtumbo kwa mambo mbalimbali kama vile elimu,afya,maji,watu wenye mahitaji maalumu,michezo na utamaduni,madaraja na barabara na elimu ya usalama barabarani.
Kawawa alisema kuwa wananchi wanatakiwa waunge mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali katika sekta zote ili kuifanya Namtumbo isonge mbele kwa maendeleo.
Akikabidhi zawadi kwa washindi katika mashindano yam waka 2022 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu alisema kuwa mashindano hayo yamefanikiwa vizuri kutokana na kampuni ya Mantra Tanzania Limited inayomiliki madini ya Uranium katika mto Mkuju uliopo Wilayani humo na Mbunge wa Namtumbo kutoa udhamini wa kutosha jambo ambalo limeongeza hamasa ya kutafuta namna ya kuanzisha timu ya Wilaya.,
Mkuu huyo ambaye ameipongeza kampuni ya Mantra na Mbunge wa Namtumbo kwa udhamini huo amesema kuwa ofisi yake inafanya kila mbinu ya kuhakikisha inakuwa na timu ya Wilaya ambayo itakayokuwa inaleta ushindani na timu zingine ikiwemo ya Nje ya Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Meneja mahusiano wa Kampuni ya Mantra Khadija Kawawa amesema kuwa kampuni hiyo imetoa udhamini wa fedha, kombe, jezi na vifaa tiba wakati wa mashindano,
Kawawa alisema kuwa Kampuni ya Mantra imekuwa ikidhamini mashindano hayo kila mwaka, pia imekuwa ikijikita kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii ambayo inaizunguka
No comments:
Post a Comment