*Asisitiza kuwa Rais Dk. Samia, Rais Dk. Mwinyi wanafanya kazi kubwa kuleta maendeleo waungwe mkono
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi
akivikwa skafu baada kuwasilikatika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa
mapokezi rasmi visiwani humo baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti
Baadhi ya Wana CCM wakiwa
katika shamrashamra za mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi yaliyofanyika kisiwani
Pemba.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza
wakati wa hafla ya mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM Zanzibar) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, iliyofanyika Mkoa wa Kusini Pemba.
NA MWANDISHI WETU, PEMBA
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM melaani kauli za baadhi ya
wafuasi, wanachama na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzi Zanzibar
zenye kuhubiri mgawanyiko na kuchochea uvunjifu wa amani.
Shaka
ameyasema hayo leo Desemba 17, 2022, wakati wa mapokezi ya Makamu
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Mwinyi yaliyofanyika kisiwani Pemba.
"Chama
Cha Mapinduzi kinalaani vikali vitendo vilivyoanza kujitokeza siku za
karibuni hasa kisiwani Pemba kwa baadhi ya wafuasi, wanachama na
viongozi wa baadhi ya vyama vya siasa kuhubiri mgawanyiko kuchochea
uvunjifu wa amani, sio utamaduni wetu wazanzibari, sio utamaduni wetu
Watanzania, CCM inalaani vikali, alisema.
Ameema
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 Ibara ya 9(a) imeahidi katika
kipindi cha miaka mitano kazi kubwa itakayofanywa na CCM ni kuimarisha
maridhiano, kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Shaka
amesema kazi hiyo inafanywa vizuri na Rais Dk. Samia na Rais Dk.
Mwinyi. "Kuweni na amani wana CCM. Hamtajutia kumwani Dk. Mwinyi kuwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, nia yake ni
kutuvusha."
Katibu
Mwenezi Shaka amesema Rais Dk. Samia na Rais Dk. Mwinyi ni nyenzo
muhimu katika kuendeleza mapatano, maridhiano na masikilizano ya kisiasa
nchini.
"Wameanza vizuri sana kwa sababu wana baraka za Chama Cha Mapinduzi," alisema.
MAMLAKA YA RAIS YAHESHIMIWE
Shaka
amesema uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar haujamwondolea
Rais Dk. Mwinyi mamlaka ya kikatiba kufanya shughuli za kiutawala.
Amesema
Dk. Mwinyi hapangiwi, bali anashauriwa na kwenye kushauriwa kuna
kukubali au kukataa, hivyo jpokuwa kuna serikali ya umoja wa kitaifa,
lakini Katiba ya nchi lazima iheshiniwe.
"Uwepo
wa serikali ya umoja wa kitaifa sio sababu ya kujihalalishia kwamba eti
kuna chama kingine ni lazima kishinde uchaguzi hapana. Wenye ulazima wa
kushinda uchaguzi ni CCM ambao tumebeba dhamana ya kuwatumikia
Wazanzibari tumebeba dhamana ya kuwatumikia Watanzania kupitia Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kazi hiyo imefanywa vizuri sana na Dk.
Mwinyi," amesema.
Aidha,
alimhakikishia Dk. Mwinyi kuwa Wazanzibari Watanzania kwa ujumla
hususan wapenda maendeleo wanamwlewa, hivyo aendelee kuchapa kazi.
"Uwepo
wa serikali ya umoja wa kitaifa sio Jukwaa la fursa na kutaka kuleta
mgawanyiko, mfarakano na kuvuruga amani ya nchi hatujafikia huko,"
alisema.
No comments:
Post a Comment