Na John Richard Marwa
Mabingwa watetezi Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL wameendeleza pumzi ya moto kwa wapinzani wake wakiikung'uta Coastal Union mabao (3-0) Uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo mtanange wa raundi ya 17 ya msimu huu wa 2022/2023.
Yanga wameingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na ubora wa kikosi chao maeneo mengi ya Uwanja sambamba na kuwa vinara wa Ligi.
Dakika ya 28 Fiston Mayele aliingia kambani kwa kuitanguliza Yanga bao lililodumu hadi dakika 45 za kwanza, akiutumia makosa ya safu ya ulinzi ya Coastal Union kushindwa kuondoa mpira alioutema mlinda mlango wao kwa shuti la Mayele.
Kipindi cha pili Yanga ni kama walikuwa wanamsukuma mlevi kutokana na ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa Coastal Union kushuka, dakika ya 47 Mayele anamalizia pasi safi ya Stephan Aziz Ki kablaa ya Feisal Salum kuandika bao la tatu na la ushindi.
Licha ya ushindi huo Yanga walicheza kwenye gia ya chini tofauti na michezo mingine msimu huu.
Coastal Union walikuwa bora kipindi cha kwanza kwa namna waivyokua wanajibu maswali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga kwa kuwa na ubora katika kuziba mianya na kufanya mikimbio sahihi wakiongozwa na Gustavo Saimon, Mtenje Albano na Aboubakary Hamza.
Coastal walikosa mawasiliano wakati wakipanga mashambulizi katika nyakati walizofanikiwa kuwashinda safu ya kiungo cha Yanga.
Kwa ushindi huo Yanga wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa NBC PL wakifikisha pointi 44 na mabao 33.
No comments:
Post a Comment