HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2023

KASKAZINI UNGUJA, ARUSHA WANG'ARA LADIES FIRST 2023


Makamu wa Rais, Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), William Kallaghe, akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu katika mbio za Mita 10000, Maycelina Mbua wa Arusha.
Mabingwa Unguja Kaskazini mara baada ya kukabidhiwa kombe lao.




 

NA TULLO CHAMBO

MKOA wa Kaskazini Unguja, Zanzibar umeibuka mabingwa katika Mashindano ya  Riadha ya Wanawake maarufu kama Ladies First, yaliyofikia tamati Januari 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Ed Salaam.

Katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyoshirikisha mikoa 30 Kati ya 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, Kaskazini Unguja, ilipata ushindani wa karibu kutoka mikoa ya Arusha na Pwani.

Kaskazini Unguja, iliibuka mabingwa baada ya kujikusanyia jumla ya medali sita, tano za dhahabu na moja ya fedha, huku Arusha ikifuatia kwa medali nane, nne za dhahabu na nne fedha.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Pwani iliyopata jumla ya medali nne, tatu fedha na  moja ya shaba.

Wanariadha walioubeba Mkoa wa Kaskazini Unguja walikuwa ni Winfrida Makenji, aliyenyakua dhahabu mbili mita 100 na 200, Jane Maige dhahabu moja mita 400, Mwanaamina Hassan Kurusha Mkuki huku pia wakinyakua dhahabu Mbio za Kupokezana Vijiti 4x100.

Kwa upande wa Arusha, Magdalena Shauri alitwaa dhahabu tatu, mita 800, 1500 na 5000 huku Jack line Sakilu akishinda dhahabu mita 10000.

Nafasi ya nne ilinyakuwa na Kusini Unguja medali nne, fedha mbili na shaba mbili huku nafasi ya tano ikienda kwa Mara medali mbili zote za fedha,Tanga nafasi ya saba medali moja ya fedha, Kilimanjaro ya saba medali moja ya shaba wakati nafasi ya nane ikinyakuliwa na Mjini Magharibi medali moja ya shaba.

Mikoa yote iliyosalia, ilitoka kapa bila medali wakati Songwe ilishindwa kuleta timu katika mashindano ya mwaka huu.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), yakiwa na lengo la kuhamasisha watoto wa kike kushiriki katika michezo hususan Riadha.

No comments:

Post a Comment

Pages