HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2023

Sanlam General Insurance yazindua Kampeni, yatoa zawadi ya Gari na Pikipiki kwa Mawakala

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insurance imezindua kampeni kabambe kwa mawakala wake ambapo washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Gari, Bodaboda na zingine nyingi kupitia Program ya Vuna Point.

 

Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi huo Meneja Masoko na Maendeleo ya Biashara, Matawi na Mawakala wa kampuni hiyo,  Charles Magori amesema lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo ni kutoa hamasa kwa mawakala wa kampuni hiyo pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

"Lengo kubwa la kuanzishwa kwa Tuzo hiI ni kutambua mchango wa mawakala wetu sambamba na zitawasaidia kuongeza ufanisi na ubunifu zaidi katika kutoaji wa huduma zao hivyo kupelekea kukua kwa mtandao wa biashara zao" Alisema Bw. Magori.

Amebainisha kuwa kampuni hiyo ambayo ina mtandao mkubwa wa mawakala ambao wanapatikana katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma, na Mbagala, Zanzibar na pia wanataraji kufungua mkoani Morogoro.

Katika hatua nyingine, Magori ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kujiunga kuwa wakala wa kampuni hiyo kujitokeza kwa wingi ambapo ameeleza kuwa wanachotakiwa kufanya ni kupiga simu kupitia namba 0800750236 na kusajiliwa kuwa wakala.

Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insurance ina  uzoefu wa zaidi ya miaka 40 ya utoaji wa huduma za bima na soko la bima nchini imekuwa ikitoa huduma za Bima za Watu na Bima za  biashara.

No comments:

Post a Comment

Pages