HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 27, 2023

TWIJUKE AWAWAKIA WANAOBEZA SAFARI ZA RAIS DOKTA SAMIA


Naibu Katibu Msaidizi Siasa Habari na Mawasiliano Chama Cha Mapinduzi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera

 

Na Lydia Lugakila Kyerwa

Naibu Katibu Msaidizi Siasa Habari na Mawasiliano Chama Cha Mapinduzi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera Tulakila Twijuke amewakemea baadhi ya watu wanaosema juu ya  Safari za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan pamoja na kukopa.

Twijuke ametoa kauli hiyo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilicholenga kujadili Rasmu ya Makadilio ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Wilaya hiyo.

Amesema hadi Sasa hakuna Mtanzania ambaye hajaona au kunufaika na Safari za Rais Dokta Samia kwani zimesaidia  kuweiweka Nchi katika ushirikiano mzuri   na Mataifa ya nje.

"Nakerwa na wanaosema Mama anasafiri sana na anakopa na tajiri huwa anakopa, na Maskini wakubwa hawakopi kwa sababu hawana maono tupunguze maneno tuangalie matendo ya Kiongozi wetu" alisema Twijuke.

Amesema Tajiri mwenye maono lazima akope na asafiri hivyo wakumbuke Rais wetu halali kwa ajili ya Watanzania wote na matokeo yanaonekana.

Aidha amempongeza Rais Dokta Samia kwa namna alivyoiwezesha Wilaya hiyo kuwa na miradi mikubwa huku akiwahimiza wasimamizi wa miradi hiyo kuitunza kwani Serikali inatumia Gharama kubwa katika Miradi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages