HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2023

Watuhumiwa wa ujambazi waliouawa na Polisi kuzikwa na Halmashauri

Na Lydia Lugakila, Ngara

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kupitia idara ya Afya wamefanya mazishi ya watu wawili waliouawa na Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia Januari 22, 2023 kwa madai ya kuhusika kwenye  tukio la ujambazi katika Kata ya Kasulo.

Afisa Afya wa wilaya hiyo Salum Kimbau amesema utaratibu wa kufanya mazishi ya watu hao umekamilika baada ya kukosa ndugu wa kutambua miili hiyo ya watu waliofariki kwa kupigwa risasi wakati wakijiandaa kufanya uhalifu.

Kimbau amesema Idara  ya Afya imesubiri  ndugu kujitokeza  bila mafanikio na kwamba miili hiyo imeharibika

Ameongeza kuwa kwa mujibu  wa sheria mtu akifariki na kukosa mtu kumtambua Halmashauri inaingia gharama za kufanya mazishi.

Hata hivyo kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo mapema Jumatatu wiki hii alibainisha kuwa watu hao wawili mara baada ya kuuawa walipekuliwa na kukutwa na Bunduki moja aina ya AK47 risasi 25 na mabomu mawili ya kurushwa kwa mkono

No comments:

Post a Comment

Pages