HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2023

Wafanyabiashara Mbagala waonywa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla leo ameongoza zoezi la usafi Wilaya ya Temeke eneo la Mbagala, ambapo amepiga marufuku ufanyaji Biashara kwenye ujenzi wa Barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa.

RC Makalla ametumia zoezi hilo kuwakumbusha Wananchi na Viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya kuhakikisha wanasimamia usafi Kila jumamos ya mwisho wa mwezi.


Aidha, RC Makalla amewaelekeza Wakurugenzi kusimamia Wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na Wakandarasi watakaoonyesha kulegalega wasipatiwe mkataba.


Pamoja na hayo RC Makalla amewapongeza Wananchi kwa mwamko mkubwa wa kufanya usafi jambo lililopelekea Jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya Sita kwa usafi Barani Afrika na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, zaidi ya Shilingi Bilioni 3.2 zimetolewa kama mkopo kwa Wafanyabiashara Wanaofanya biashara kwenye Maeneo Rasmi na kutoa wito kwa Wafanyabiashara wengine kuacha kufanya biashara holela.

No comments:

Post a Comment

Pages